August 28, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mambo matano ya Mwabukusi aliyomwambia Rais Samia

 

Leo nimefika Ikulu ya Chamwino kuwasilisha majumuisho ya wadau mbalimbali, ambapo tulipata nafasi adhimu ya kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwasikisha kwa Mukhtasari kuhusu masuala makuu ya kitaifa yanayohusu:

1. Utawala Bora na Demokrasia – tukisisitiza umuhimu wa kuweka mifumo thabiti inayohakikisha heshima ya utawala wa sheria, uwajibikaji na uwazi.

2. Haki za Ushiriki katika Chaguzi tukieleza haja ya kuwa na uchaguzi unaozingatia haki za wananchi, ushiriki huru wa wagombea, na kuondoa vikwazo vya kiufundi vinavyoweza kunyima wananchi na wagombea haki ya kidemokrasia.

3. Changamoto za Utekaji na Kutoweka kwa Watu (Enforced Disappearances) tukimueleza Rais juu ya umuhimu wa kulinda haki za msingi za raia kwa kuzuia vitendo hivi visivyo vya kisheria.

4. Maboresho ya Mfumo wa Uchaguzi tukihimiza mageuzi yatakayowezesha chaguzi zilizo huru, haki na shirikishi, ili wananchi wapate viongozi wanaowataka kupitia sanduku la kura bila hila wala vizuizi visivyo halali na kuondoa changamoti ya kukata wagombea au kuzuia Mawakala.

5. Suala la Tundu Lissu tuliliwasilisha kwake na linaendelea kuangaliwa na kufanyiwa kazi kwa utaratibu mwingine lakini bila kuingilia kinachoendelea Mahakamani

Rais alitusikiliza kwa makini na akatoa ahadi ya kuangalia kwa karibu mapendekezo yaliyotolewa, ili kuona namna bora ya kuyatekeleza kadri muda na mazingira yanavyoruhusu.

Aidha, kwa kuwa mapendekezo hayo yamegawanyika katika ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu, Rais ameahidi kuyapitia kwa ukamilifu na kuchukua hatua stahiki kwa yale yatakayowezekana, ili kuhakikisha Taifa linaingia kwenye uchaguzi ulio bora zaidi, wenye heshima, uhuru na haki kwa Watanzania wote.

Mwabukusi

About The Author

error: Content is protected !!