April 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Tundu Lissu agoma kusikiliza kesi yake kwa njia ya mtandao

Tundu Lissu, Mwenyekiti Chadema

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amegoma kusomewa maelezo ya awali katika kesi kusambaza taarifa za uongo mtandaoni kwa njia ya mtandao ‘video conference’. kutokea katika Gereza la Ukonga alipo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo imesikilizwa leo tarehe 24 Aprili 2025, kwa njia ya mtandao ambapo Upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema ulidai kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya Lissu kusomewa Maelezo ya Awali (Ph).

Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulipoulizwa mbona mshtakiwa Lissu haonekani mtandaoni, Hakimu Mhini alimtaka Askari Magereza ajibu ambapo alisema kwamba Lissu amegoma kusomewa maelezo ya awali kwa njia ya mtandao (visual) ambapo Hakimu Mhini alirihusu kesi kuendelea bila Lissu kuonekana.

Lissu amegoma kutokea mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geofrey Mhini wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam aliyekuwa akiendesha kesi hiyo kwa njia ya mtandao.

Kesi hiyo ilichelewa kuendelea kwa njia ya mtandao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuanzia saa 3:15 hasi 3:59 asubuhi baada ya mitambo kusuasua.

Vijana wa Mahakama wa masuala ya Tehema walihaingaika kwa muda kwa ajili ya kuwaunganisha kwenye mtandao Mawakili wa Serikali, Gereza la Ukonga alipokuwa Lissu na Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini pamoja na mawakili wa utetezi ili waweze kusomana.

Ilipofika saa 3:24 asubuhi Hakimu Mhini alianza kwa kuita tena ili apate uthibitisho kama Lissu yupo mahakamani na pia kama mawakili wa Serikali wanamsikia, askari wa Jeshi la Magereza aliyeonekana kutoka Ukonga alimuomba hakimu kama dakika mbili wamlete, kwa hiyo aliomba Mahakama ivumilie kidogo.

Baada ya kauli hiyo, baadhi ya watu wakaanza kunong’ona kwa sauti ndipo Hakimu Mhini alipowaeleza kwamba waache kelele na ilipofika saa 3:33 asubuhi hakimu aliwaita tena askari Magereza kama wapo tayari .

Ndipo mmoja wa Mawakili wa Lissu kati ya mawakili zaidi ya 25, Mpare Mpoki alimueleza hakimu kwamba wanapoteza muda wakati vitabu vipo yaani Mwenendo w Makosa ya Jinai (CPA).

“Kama ripoti ya kiufundi ipo basi nipate taarifa nifanye uamuzi,” amesema Hakimu Mhini.

Kijana mmoja wa Tehama wa Mahakama akamueleza hakimu kwamba tayari wameshawasiliana nao. Saa 3:45 asubuhi Magereza wakauganishwa, ambapo Hakimu Mhini alisema anatoa dakika 10 tu zikipita basi atafanya uamuzi.

“Haya Magereza mnanisikia, mawakili.wa Serikali mnanisikia? Mpo tayari? Ndiyo naona mtandao unasumbua,”Amesema Hakimu

“Sisi tupo tayari kuendelea kwa wote sababu wote walikuwa wanajua tarehe ya kesi,” amedai Wakili Mpoki.

Hakimu Mhini alimjibu kwanza hawezi kuendelea hadi awapate pande zote mbili na ilipofika saa 3:59 asubuhi Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliieleza Mahakama kuwa wapo tayari kuendelea na askari Magereza amedai kwamba walipomfikishia taarifa Lissu amedai kwamba hawezi kuendelea kwa njia ya mtandao.

Baada ya mitambo kukaa sawa ndipo kesi ikaendelea ambapo pamoja na mambo mengine upande wa utetezi uliwasilisha mapingamizi mbali mbali Miongoni mwao ikiwamo wanapinga utaratibu wa kesi hiyo kusikilizwa kwa njia ya mtandao huku wakitaka mtuhumiwa afikishwe mahakamani kwani ili asomewe Maelezo ya Awali (Ph) lazima Upande wa Jamhuri, utetezi na mtuhumiwa wawepo mahakamani sambamba na mtuhumiwa kusaini karatasi ya maelezo.

“Hata kama mtuhumiwa angekuwepo mtandaoni (visualizer) leo tusingeweza kuendelea kwa sababu ingekuwa ni kinyume na sheria kwa sababu sheria inataka maelezo ya awali yafanyike mtuhumiwa akiwepo,” amedai Wakili Mpoki.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi hadi tarehe 28 April 2025, ambapo itakuja kwa ajali ya upande wa Jamhuri kujibu mapingamizi hayo.

Katik kesi hiyo inadaiwa a kuwa tarehe 3 Aprili mwaka huu, jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulaghai umma, alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka, ‘Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana, wagombea wa Chadema walienguliwa kwa melekezo ya Rais.’

Maneno mengine yalisomeka ‘Mapolisi wanatumika kuiba kura wakiwa na vibegi, pia alichapisha maneno yaliyosomeka ‘Majaji ni Ma-CCM hawawezi kutenda haki wanapenda wapate teuzi kuchaguliwa kuwa majaji wa Mahakama ya Rufaa’.

About The Author

error: Content is protected !!