
Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti Chadema Bara
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa kimeambiwa na Jeshi la Magereza kuwa Mwenyekiti waoTundu Lissu amehamishwa katika gereza la Keko na sasa yupo katika Gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa ya Chadema ya leo tarehe 19 Aprili imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Brenda Rupia na kueleza kuwa Lissu yupo Ukonga.
Rupia anaeleza kwenye taarifa yake kuwa chama hicho kimezungumza na jeshi la Magereza na kuelezwa kuwa Mwenyekiti wao yupo salama.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho atamtembelea Lissu gerezani Ukonga leo tarehe 19 Aprili.
ZINAZOFANANA
Mbezi juu yashikwa mkono na Meridianbet
Serikali yajivunia mafanikio sita ya TASAF
Dk. Kimei aweka rekodi ya utendaji Vunjo