April 15, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Majaliwa ataja ukuaji na mapato ya reli ya kati

 

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kwanzia Agosti Mosi 2024 mpaka Februari 2025 kwenye huduma ya usafiri wa reli kati ya Dar es salaam – Morogoro – Dodoma jumla ya abiria 1,809, 983 wamesafirishwa na kiasi cha Sh. 54.9 bilioni zimekusanywa. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dodoma … (endelea).

Amebainisha hayo leo tarehe 09 Aprili, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akitoa hotuba yake ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Bunge kwa mwaka 2025/2026.

“Uwepo wa huduma hiyo ya treni, umepunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma kutoka wastani wa saa 10 kwa basi hadi kati ya saa tatu na nne na kuchagiza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa nchini,” amesema Majaliwa.

Aidha Majaliwa amesema kuwa serikali inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa ambapo hadi kufikia Februari 2025 Ujenzi kipande cha kutoka Mwanza- Isaka 341km umefikia asilimia 62.37, Makutupora-Tabora 368km umefikia asilimia 14.35, Tabora- Isaka 165kmumefikia asilimia 6.33 na Tabora- Kigoma 506 km umefikia asilimia 7.3.

Majaliwa amesema kuwa maandalizi ya kuanza ujenzi wa kipande cha Uvinza- Malagarasi – Musongati 282km yameshaanza ambapo serikali ya Tanzania na Burundi zimesaini Mkataba wa Ujenzi wa kipande hicho siku ya tarehe 29  Januari, 2025.

About The Author

error: Content is protected !!