
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo, amtoa wito kwa taasisi za serikali kuweka vipaumbele katika kuboresha miundombinu hasa kwenye maeneo yenye vyanzo vya kiuchumi kama vile maeneo ya uwekezaji. Anaripoti Apaikunda Mosha, Njombe … (endelea).
Aliyasema hayo jumatatu tarehe 24 Machi 2025 baada ya wa uzinduzi wa Ofisi ya Kanda ya Nyasa ya kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) iliyoko Njombe ambao unatajwa kuwa sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha kuwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi wanapata huduma bora na kwa ukaribu zaidi.
Amesisitiza pia umuhimu wa TIC kutoa huduma bora na za kina kwa wawekezaji katika kanda hiyo. Aidha ameiagiza TIC kuhakikisha kuwa wawekezaji hawakumbani na changamoto zisizo za lazima katika shughuli zao za uwekezaji hivyo amewataka kuonyesha ushirikiano na ofisi za halmashauri ili waweze kuwasaidia wawekezaji kwa ufanisi zaidi.
Mara baada ya uzinduzi huo, Mkumbo alitembelea na kukagua wawekezaji mbalimbali waliopo katika mkoa huo, ikiwemo kiwanda cha Murikado food supply Co. Ltd ambacho kinachakata mafuta ya parachichi.

Akiwa katika kiwanda hicho, Mkumbo alimpongeza mwekezaji huyo, ambaye ni Mtanzania aliyewekeza na kuona fursa katika sekta ya kilimo hadi uchakataji wa mafuta na amewataka wafanyakazi kulinda mali za viwanda ili kuhakikisha vinaendelea kunufaisha Watanzania kwa kuchochea ajira na uchumi wa nchi.
Alisisitiza kuwa huduma za msingi kama maji, barabara, na umeme ni muhimu mno kwa mwekezaji, amesema mwekezaji hapaswi kuhangaika kuhusu huduma hizi, kwani anakuja kuzalisha ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa eneo husika.
Aidha, hafla ya uzinduzi wa kituo hicho ilihudhuriwa na viongozi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TIC Binilith Mahenge, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Gilead Teri, Wakuu wa Wilaya, wawekezaji na wafanyabiashara wa mkoa wa Njombe.
ZINAZOFANANA
GF Automobile, NaCoNGO zasaini makubaliano ya kimkakati
WMA yajivunia kuongezeka kwa ajira nchini
NEMC kupambana na magugu maji Ziwa Victoria