
Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Nyakaho Mahemba
KATIKA mwaka wa fedha 2024/25 mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania umepata ongezeko la Sh. 3 bilioni tofauti na mwaka wa fedha 2023/24 ambapo ulikuwa na bajeti ya Sh. 1.6 bilioni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, Nyakaho Mahemba,alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya utekelezaji na maendeleo ya mfuko huo kwa muda wa miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Akielezea mafanikio hayo Nyakaho, amesema kuwa awali bajeti ya mfuko huo ilikuwa chini ya kiwango cha uendeshaji na uboreshaji wa mfuko,suala lililokuwa likipunguza ufanisi wa utendaji.
Mtendaji huyo amesema kuwa tangu kupatikana kwa uhuru mfuko huo haujawahi kuwa na bajeti kubwa kama ilivyo kwa sasa.
Amesema kuwa sekta ya utamaduni ilikuwa ikipata ruzuku ya Sh. 500 milioni ambayo ilikuwa haiwezi kukidhi malengo ya sekta hiyo na baadaye katika mwaka fedha 2023/24 iliidhinishwa bajeti ya Sh. 1.6 bilioni na mwaka wa fedha 2024/25 ikaidhinishwa Sh. 3 bilioni jambo ambalo halijawahi kutokea katika sekta hiyo.
Aidha, amesema kuwa kiasi kilichoongezeka ni Sh. 1.4 bilioni ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 87.5 huku Serikali ikiongeza chanzo kipya na endelevu cha mapato ya Mfuko kinachotozwa katika vibebeo tupu vya Kazi za Sanaa (Tozo ya Hakimiliki – Copyright Levy).
Ameeleza kuwa kupitia chanzo hichi, Mfuko hupata gawio la asilimia 10 ya mapato yote yanayokusanywa na chanzo hiki kimeanza kutekelezwa Mwezi Septemba, 2023.
Katika hatua nyingine amesema kuwa Mfuko umefanikiwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Mikopo yenye thamani ya Shilingi 5,250,070,500.89 kwa miradi 359 ya Sanaa iliyozalisha jumla ya ajira 497,213.
Akielezea mchanganuo wa miradi aliyataja maeneo ya miradi iliyowezeshwa ni muziki (miradi 78), filamu (miradi 90), maonesho (miradi 65), Ufundi (miradi 103) na Lugha na Fasihi (23).
Pia ameitaja Mikoa iliyofikiwa ni 18 ambayo ni Dar es Salaam, Arusha, Morogoro, Pwani, Geita, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Kagera, Mara, Shinyanga, Tabora, Singida, Manyara, Kilimanjaro, Simiyu, Kigoma na Katavi.
ZINAZOFANANA
Wananchi wa Mahomanyika wampigia magoti Rais Samia mgogoro wa ardhi
Mapungufu ya usimamizi wa rasilimali watu, waajiri watajwa
Serikali yaboresha vyuo 33 katika kipindi cha mwaka 2021/24