
MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufunzi Stadi (VETA), Anthony Kasore amesema serikali kwa mwaka 2021/2024 ilitenga kiasi cha Sh. 233.7 bilioni kwa ajili ya kufanya maboresho na ujenzi wa miundombinu ya VETA hapa nchini. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dodoma … (endelea).
Hayo ameyasema Jumatatu ya tarehe 3 Machi 2025, wakati anatoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu na mafanikio ya mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa mwaka 2021/24.
Kasore amesema, tangu uanzishwaji wake mwaka 1994 VETA ilipewa majukumu ya kuhakikisha kwamba inasimamia, kugharamia na kuratibu ufunzaji wa elimu ya ufundi stadi nchini, ili kuwe na mafundi mahiri wakutosha katika kutekeleza majukumu ya shughuli mbalimbali zinazohitaji rasilimali watu wenye ujuzi.
Akiainisha miradi mbalimbaliya maendeleo iliyofanywa na inayoendelea kufanywa amezungumzia kukamilika kwa ujenzi wa vyuo 33 katika wilaya 29 na mikoa minne, uliogharimu takribani bilioni 94.5, sambamba na hilo serikali imeendelea kuhakikisha ujenzi wa vyuo 64 unaendelea katika maeneo mbalimbali na tayari imetoa bilioni 103 kwa mradi huo.

Ameeleza pia, maboresho ambayo serikali imefanya katika vyuo vya VETA amesema kiasi takribani biloni 14.2 imetolewa kwa ajili ya maboresho katika vyuo ndani ya wilaya mbalimbali, na kwenye manunuzi ya vifaa vyenye ubora na vinavyokidhi mahitaji kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia, takribani bilioni 22 zimetolewa ili waweze kukidhi mahitaji ya soko la ajira.
Aidha maboresho mengine ni kwenye uboreshaji wa mitaala 42, pamoja na kutengeneza mingine mipya 20 ambayo inajumuisha TEHAMA, michezo, umeme, magari, mitambo, kilimo, ukarimu, usafirishaji, biashara, mavazi, madini na urembo ili wawe na uwezo wa kujitengenezea kipato na kuliingizia taifa kipato.
Ameeleza pia katika vyuo vya kurekebisha tabia (magereza) jumla ya watu 214 katika vituo vya Ukonga, Arusha na Morogoro wameweza kufanyiwa tathmini ya ujuzi wao, na wamepatiwa vyeti ili waweze kuaminika nakufanya kazi ya kuridhisha.
Aidha katika program ya urasimishaji ujuzi ya Rais Samia amesema mpaka sasa wameshafanya urasimishaji wa watu 1600 na mpaka ifikapo juni 2026 wanatarajia kuwafikia zaidi ya wananchi 80,000 ili kuhakikisha uwa watu wanatambulika na wanapata zabuni mbalimbali.
Kasore ameeleza namna ya upatikanaji wa mafunzo kutokana na teknolojia muhitaji hatafika chuoni amesema, unaweza kusoma katika mifumo kama mfumo wa visomo mpaka atakapohitajiwa kufika chuoni kusoma kwa vitendo, mafunzo kwa masafa pamoja Akili unde (Artificial Intelligence).
Sambamba na hayo amesema matarajio ya VETA ni kutoa tunuku za kimatafa ili kumuhakikishia mtu kupata kupata fursa za ajira maeneo mengi, amesema kutakuwa na vyuo vya kimataifa 14 ambavyo vitatoa mafunzo hayo na viwili kati ya hivo tayari vimeeanza kazi ya utoaji wa elimu ya uungaji wa vyuma.
ZINAZOFANANA
GF Automobile, NaCoNGO zasaini makubaliano ya kimkakati
WMA yajivunia kuongezeka kwa ajira nchini
TCI yafungua ofisi Njombe, kuleta huduma za uwekezaji karibu