WAKATI Dunia ikienda kasi katika teknolojia Tanzania itanufaika na ushikiano wa Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania kupitia programu yake ya FUNGUO, Vodacom Tanzania, na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) ambapo ushirikiano huo umefanikisha kuandaa Wiki ya Ubunifu Tanzania 2025 (IWTz2025). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
ushirikiano huu utazidi kuimaisha Tanzania kwenye maendeleo ya Teknolojia na ubunifu. Wiki hiyo itakayoanza tarehe 12 Mei mpaka tarehe 16 Mei 2025 katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam. Wakati huo huo kutafanyika mkutano wa Future Ready wa Vodacom.
Kauli mbiu ya mkutano huo itakuwa “Ubunifu kwa Maendeleo Jumuishi na yenye Ustahimilivu”, ikilenga kuonyesha dhamira ya pamoja yakujenga jamii endelevu, jumuishi na ya kisasa katika kutatuachangamoto ya ajira kwa vijana kwenye zama hizi za kidijitalina kuchochea ukuaji wa kibiashara kupitia tafiti na ubunifu.
Leo tarehe 5 Februali 2025 Taasisi hizo zimetangaza ushikiano huo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Phillip Besiimire amesema ushirikiano huo utaleta mabadiliko katika sekta ya ubunifu nchini Tanzania, kwa kuunganisha wabunifu na wajasiriamali wa kimataifa kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
“Tunalenga kuleta mitazamo na taaluma za kimataifa kwenye mijadalahii na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha mabadiliko yakidijitali, sambamba na kuanzisha mifumo ya ikolojia yaubunifu inayoongozwa na vijana.
“Jitihada za Vodacom za kutumia teknolojia kwa lengo la kuboresha maisha ndiozinazounda msingi wa ushirikiano huu unaoendeshwa na maonoyanayofanana ya kuwawezesha watanzania kuendelea kupitiaUchumi wa kidijitali ulioendelevu na jumuishi.”
Aidha amesema kuwa mkutano wa Vodacom wa Future Ready Summit (FRS2025) ni tukio linaloweka msingi wa maadhimisho hayo pamoja nakuibeba kauli mbiu ya “Kubadilisha hatma ya miji: Usasa, Uendelevu na Jumuishi”, ambayo inazungumzia umuhimu wa kuibadili miji ya Tanzania kwa ajili ya kutatua changamoto zinazotokana ukuaji wa kasi, mabadiliko ya tabia nchi namabadiliko ya teknolojia.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa UNDP Tanzania, Shigeki Komatsubara, amesisitiza dhamira ya UNDP ya kujenga mfumo wa ubunifuulio jumuishi na wenye ustahimilivu.
“Tunatambua kuwa ubunifu ni nyenzo muhimu katika kushughulikia changamoto za maendeleo endelevu na kuunda fursa shirikishi.Kupitiaushirikiano huu, tunalenga kuwainua Watanzania, hasa vijana nawanawake, kuwa chachu ya mabadiliko chanya.
“Wiki ya Ubunifu Tanzania 2025 (IWTz2025) itaonyesha ari ya ubunifuTanzania kwenye jukwaa la kimataifa, kuvutia uhamasishaji naushirikiano kupitia na mifumo iliyofanikiwa duniani.”
Kuhusu ajenda zitakazohusika katika maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu ni hayo itahusisha mijadala mtambuka, warsha na maonyesho, huku lengo likiwa ni Mustakabali wa miji mahiri, endelevu na jumuishi, Uwezeshaji wa vijana kwenye zama za kidijitali, Uboreshaji wa tafiti na ubunifu kwa ajili ya biashara
Akizungumza kwa niaba ya Serikali, Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo na Uhamisho wa Teknolojia kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk Athumani Ngumia alisema mchango muhimu wa ushirikiano huo ni kukuza ubunifu.
“COSTECH imejidhatiti kuwaunganisha wadau kwa lengo la kuchochea utafiti, teknolojia na ubunifu ambao unaendana navipaumbele vya nchi katika maendeleo na maono ya mwaka2050.Maadhimisho ya Wiki ya Ubunifu kwa mwaka 2025 nijukwaa pekee kwa ajili ya sekta binafsi na umma kupeleleza nakutekeleza masuluhisho kwa ajili ya ukuaji endelevu.”
Wiki ya ubunifu 2025 (IWTZ2025) na mkutano wa Future Ready Summit (FRS2025) inatarajia kuwaleta pamoja washiriki, wazungumzaji na wabunifu kutoka Tanzania, Afrika na sehemu mbalimbali duniani na kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana maarifa, kuendeleza ushirikiano wenye tija na kuhamasishamawazo yenye kuleta mabadiliko.
Washiriki wa matukio haya wanahamasishwa kutekeleza shughuli mbalimbali sambamba na matukio hayo muhimu kwa lengo la kuhakikisha watu wengi zaidi nchini wanawezakunufaika na mikutano hiyo itakayo kuwa inafanyika kwenyeKituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.
Wakati huo huo Meneja Program kutoka FUNGUO Joseph Manirakiza ametumia nafasi hiyo kuelezea kwa kina umuhimu wa ushirikiano huo sambamba na kutambua mchango wa bunifu katika kukuza maendeleo endelevu
Kuhusu Programu ya FUNGUO ni kwamba inajitolea kuendeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) nchini Tanzania kwa kutumia mbinu shirikishi inayolenga kusaidia maendeleo ya biashara bunifu na zinazozingatia athari chanya kwa jamii, hususan kwakuimarisha mazingira ya ubunifu kwa wajasiriamali na biasharandogo na za kati (MSMEs).
Aidha FUNGUO inatambua kuwa kusaidiana kukuza biashara hizo siyo tu kutachangia kuongeza ajira, hususan kwa wanawake na vijana, bali pia kutaboresha kipato, kuboresha hali ya maisha, na kuchochea maendeleo jumuishi naendelevu.
Pia Mpango huo unafadhiliwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya(kupitia Mpango wa BEGIN), Serikali ya Uingereza (kupitiaMpango wa Ushirikiano wa Teknolojia na Ubunifu barani Afrika – ATIP), na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP).
FUNGUO unatekelezwa na UNDP Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji wa Umoja waMataifa (UNCDF). Ushirikiano huu wa wadau mbalimbali unahakikisha ufanisi na athari chanya katika mazingira yaubunifu nchini Tanzania.
Kwa kushirikiana kwa karibu na Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH) pamoja nataasisi nyingine za serikali, FUNGUO inalenga kuchangia maendeleo endelevu nchini kwa kuweka mazingira wezeshi kwabiashara bunifu na MSMEs.
Kuhusu Vodacom Tanzania ni mtoa huduma wa mawasiliano anaeongoza nchini Tanzania, ikiwa na mtandao wa data wa kasi zaidi. Tunahudumia zaidi ya wateja milioni 26.3. Vodacom Tanzania na kampuni zake tanzu ni sehemu ya Vodacom Group yenye usajili nchini Afrika Kusini, ambayo nayo inamilikiwa naVodacom Group Plc yenye makao makuu Uingereza.
Wakati COSTECH ni Tume ya Sayansi na Teknolojia Tanzania iliyoanzishwa kupitia Sheria ya Bunge Na. 7 ya mwaka 1986.Pia ni shirika la umma linalohusika na kuratibu na kukuza shughuli za utafiti na maendeleo yateknolojia nchini.
Pia, inatoa ushauri kwa serikali kuhusumasuala yote yanayohusiana na sayansi, teknolojia, na ubunifu(STI) kwa lengo la kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamiinchini Tanzania.COSTECH inafanya kazi chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
ZINAZOFANANA
Cheza Sloti ya Spin Spin Sugar mchezo mpya wa kasino
Ewura watangaza bei mpya ya mafuta
Kasino ya Coin Strike Hold & Win inakupa ushindi rahisi