TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ametangaza nia ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa hicho. Amesema kuwa atafanya mabadiliko kadhaa ambayo anayaona na mapufu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu akitangaza Rasmi uamuzi huo leo amesema ametangaza uamuzi huu baada ya kujiona anasifa zilianishwa na Katiba ya chama hicho ikiwa pamoja na msimamamo wa kuaminika.
Lissu amesema kuwa mapito aliyepitishwa ikiwa pamoja na kushambuliwa tarehe 7 September 2017 jijini Dodoma pamoja na kunyang’anywa ubunge wake bila kupewa stahiki zake.
Lissu ameizungumzia kuboresha katiba ya chama hicho ikiwa pamoja na ukomo wa uongozi ili kuyaenzi maono ya Mwenyekiti wa Kwanza wa chama hicho, Edwin Mtei na aliyefuata Bob Makani.
“Ukomo wa madaraka utapunguza upambe na uchawa unaoshamiri kwa viongozi wanaong’angania madaraka”
Lissu amesema kuwa jambo jingine la kurekebisha ni mifumo ya uchaguzi ndani ya chama ili kudhibiti uhuni na rushwa.
Lissu amesema kuwa nyakati zimebadilika ni lazima mbinu za kukikabili Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pia Lissu amesema kuwa chama hicho kitabadilisha mfumo wa fedha kutoka kwenye umiliki wa mtu mmoja.
ZINAZOFANANA
Bilionea na kiongozi wa kiroho Aga Khan afariki dunia
Ndoa ya Ramovic na Yanga yavunjika baada ya siku 80
Kagame, Tshisekedi, uso kwa uso Dar es Salaam