MKURUGENZI wa Miradi ya Green Faith Duniani Meryine Warah amewashauri viongozi wa madhehebu mbalimbali nchini kutofumbia macho vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vinavyojitokeza katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kule Chongoleani mkoani Tanga. Anaripoti Mary Victor, Dar es Salaam … (endelea).
Maryine aliyesema katika mkutano wake na wadau wa mazingira uliofanyika hivi karibuni jijini ambapo pamoja na mambo mengine aliwashauri viongozi wa dini kutokujiweka pembeni mambo yanapoharibika kutokana na kwamba imani ya wananchi ipo kwa wa kiimani.
“Kumekuwa na malalamiko mengi katika mradi wa bomba la mafuta kwa watu kuondolewa katika makazi yao ya asili na kutofidiwa ipasavyo lakini hakuna sauti ya viongozi wa dini wanaokemea hali hiyo kwa kuiambia serikali ukweli . Watu wa dini mnapaswa kahusika katkka mambo ya mazingira kwa sababu ni wito”
Kwa mujibu wa Meryine ni muhimu kuelewa na kuzingatia umuhimu wa kutunza mazingira. Na muhimu sana kutetea haki za jamii, viongozi wanalo jukumu la kuwalinda wananchi.
“Kuna wakati najiuliza viongozi wa dini mbona mmenyamaza? Nafurahi kule nchini Kenya sasa hivi mwanasiasa wakiwaletea fedha kwa ajili ya kusitisha jambo fulani wanazirudisha hadharani”
Naye mkazi wa Wilaya ya Mkingq Tanga Shekhe Abuubakar Galbu alisema tayari vijiji vitatu vimefutika na waliokuwa wanaishi kwenye maeneo yale hawana malazo maalum ya kuishi.
Miongoni mwa vijiji hivyo ni pamoja na Putin, Nahoya na Chongoleani. Mradi unanufaisha zaidi kampuni za Magharibi huku tukibaki kutengeneza taifa la watu masikini
“Wakati mradi unakuja tulielewa kwamba sisi tutafaidika, mimi nikaambiwa niboreshe ofisi maana nitauza sana tofali lakini sivyo ilivyo. Njaa imeongezeka zaidi Kumekuweko na ongezeko kubwa na ukataji minazi ambalo kwetu ni zao la biashara
“Tulikuwa tunazungumza kama hadithi lakini sasa hivi tunashuhudia uhalisia”
ZINAZOFANANA
Bashungwa apokelewa wizara ya Mambo ya Ndani Zanzibar
Tuendelee kutumia teknolojia katika uhifadhi – Dk. Abbasi
Wanandoa waiomba Mahakama Kuu ipitie mwenendo wa kesi yao Kisutu