TANZANIA inajiandaa kurusha Satelaiti ya kwanza itakayolinda mipaka na Bayoanuwai katika hifadhi na mapori nchini. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam …(endelea).
Satelaiti hiyo iliyopewa jina la TanSar1, imetengenezwa na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT); na ikashinda shindano la raundi ya nane la KiboCUBE la dunia la kurusha Satelaiti.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 28 Oktoba 2024, kupitia kurasa za mitandao ya kijamii ya Wizaraya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, imesema kuwa wizara hiyo imeratibu ushiriki wa DIT kwenye shindano hilo lilofanyika tarehe 30 Julai 2024 na DIT kutawazwa kuwa washindi.
Taarifa hiyo imesema kuwa Serikali imeamua kuitumia Teknolojia hiyo kwa ajili ya ulinzi wa mipaka na bayoanuwai katika hifadhi na mapori ya akiba nchini.
Taarifa hiyo imesema kuwa hilo lilikuwa ni agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alilolitoa jijini Dar es Salaam, tarehe 17 Oktoba 2024 alipokuwa akifungua kongamano la nane la Tehema Tanzania.
“Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) inajiandaa kuanza mradi wa utafiti utakaopelekea kutengeneza na kurusha satelaiti (TanSat1).
TanSat1 itakuwa na jukumu la kulinda mipaka na bayoanuwai katika Hifadhi na mapori kwa kuiwezesha Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania (TAWA), kufuatilia na kukusanya taarifa kwa kutumia vifaa maalumu ili kuhakikisha uhai wa viumbe na afya ya mifumo ya ikolojia inaimarishwa.”
Aidha, imesema hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST), zimeweka mipango ya kuendeleza kada ya wataalam wa anga.
ZINAZOFANANA
Serikali yaipa ITA jukumu la utafiti wa mapato
Benki ya NBC yatambulisha kampeni ya Kilimo Mahususi kwa wakulima na wafugaji Mbeya
Upelelezi wakwamisha kesi ya Boni Yai