RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Mwinyi, amewaapisha Wakuu wa Wilaya aliowateua hivi karibuni.Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea). Hafla hiyo ya uapisho imefanyika leo tarehe 13 Aprili 2026, Ikulu Zanzibar, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wanafamilia wa Wakuu wa Wilaya walioapishwa. Walioapishwa ni pamoja na, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A, Lailah Burhani Ngozi, Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Dk. Said Haji Mrisho, Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Ali Abdalla Said Natepe, Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Riziki Daniel Yussuf, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Zuhura Mgeni Othman. Hafla hiyo imehudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla,Jaji Mkuu wa Zanzibar, Khamis Ramadhan Abdalla, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dk. Mwinyi Talib Haji,Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kaabi,Wakuu wa Mikoa pamoja na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Kamala Harris kuwania Urais Marekani 2028 ACT yawasilisha Ripoti ya Uchaguzi uliovurugwa