KAMALA Harris, ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Merekani kutoka Januari 2021 hadi Januari 2025 chini ya Joe Biden, ametangaza kuwa anaweza kugombea tena Urais mnamo 2028. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Mgombea huyo wa Chama cha Democratic alitoa tangazo hilo mnamo 10 Aprili 2026, alipokuwa akihudhuria Mkataba wa National Action Network Convention, Shirika la kutetea haki za kiraia lililoanzishwa na mchungaji Al Sharpton.
Hafla hiyo iliyohudhuriwa na watu wengi huko Manhattan, New York, Marekani, Harris alisema kuwa bado ana nafasi ya kuiongoza Marekani.
Kamala Harris alikuwa mgombea katika uchaguzi wa Marekani wa 2024, akichukua nafasi ya Joe Biden, uchaguzi ambao Donald Trump alishinda.
Kwa ujumla, Trump alimshinda Kamala Harris kwa zaidi ya kura Milioni Mbili.
ZINAZOFANANA
Tume ya 29 Oktoba yakutana na Rais Chakwera
Guelleh ashinda Urais Djibouti kwa muhula wa sita mfululizo
Marekani yakanusha taarifa za kuachiwa kwa mali za Iran