RAIS wa Ismail Omar Guelleh (78) ameibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Djibouti, baada ya kupata asilimia 97.81 ya kura zilizopigwa. Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Ushindi huo unamuwezesha Guelleh kuendelea kuiongoza nchi hiyo kwa muhula wa sita mfululizo, akiendeleza utawala wake ulioanza tangu mwaka 1999.
Katika mabadiliko ya kikatiba yaliyofanyika mwaka 2025, kipengele cha ukomo wa umri wa juu wa kugombea urais kiliondolewa, ambapo hapo awali mgombea hakutakiwa kuzidi miaka 75.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa ilifungua njia kwa Guelleh kuwania tena nafasi hiyo ya juu ya uongozi, licha ya umri wake wa sasa.
ZINAZOFANANA
Kamala Harris kuwania Urais Marekani 2028
Tume ya 29 Oktoba yakutana na Rais Chakwera
Marekani yakanusha taarifa za kuachiwa kwa mali za Iran