WATU wawili wamefariki dunia huku wengine watatu hawajulikani waliopo baada ya jahazi la mizigo kupoteza uelekeo na kuzama katika eneo la Nungwi wakati jahazi hilo likielekea Bandari ya Mkokotoni visiwani Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Ajali hiyo ilitokea 14 Machi wakati jahazi hilo lilipokuwa likitoka Bandari ya Pangani Mkoani Tanga kuelekea Bandari ya Mkokotoni visiwani Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, miili ya watu wawili tayari imepatikana katika maeneo ya Mkokotoni bandarini.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mhandisi Christopher Mlelwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Mlelwa amesema jahazi hilo lilikuwa likijulikana kwa jina la MV Talawanda na lilikuwa likifanya safari zake kati ya Pangani na Mkokotoni kwajili ya kubeba mizigo.
“Kimsingi tunasisitiza vyombo vyote vinavyosafiri kwa njia ya maji vinatakiwa kusajiliwa na kuthibitishwa ubora na mamlaka husika ambayo ni TASAC,” almesema Mlelwa.
Pia ameeleza kuwa chombo hicho kilisajiliwa kwa ajili ya kusafirisha mizigo pekee na si kubeba abiria.
ZINAZOFANANA
Kondomu kupanda bei
Hatutaongeza bei ya gesi – Taifa Gas
Prof. Kabudi amrihi Lukuvi, Mgombea Mwenza wa NCCR- Mageuzi, azawadiwa ubunge