January 31, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Uwekezaji wa Samia, wanafunzi 16 wasomea Data Science na AI Afrika Kusini

 

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza utekelezaji wa vitendo wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwekeza kwenye sayansi na teknolojia, baada ya kuwaaga wanafunzi 16 waliopata ufadhili wa masomo ya juu nje ya nchi kupitia mpango wa ‘Samia Scholarship’. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wanafunzi hao wanaelekea Chuo Kikuu cha Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa masomo yanayolenga kuzalisha wataalamu bingwa katika sayansi ya data, akili unde (Artificial Intelligence) na teknolojia ya viwandani.

Akizungumza wakati ghafla ya kuwaaga wanafunzi hao leo tarehe 30 januari 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoloji Profesa Adolf Mkenda, amesema kuwa ufadhili huo umelenga kuongeza wataalamu kwenye sayansi ya data, akili unde , na teknolojia ya viwanda.

Mnakwenda Afrika Kusini kwa ufadhili wa masomo ambayo Rais Samia aliuagiza nasi tunatekeleza na sisi tumeuita ‘, wanafunzi wa hawa 16 kati ya wanafunzi 50 waliofanya vizuri mitihani ya kidato cha sita kwenye masomo ya sayansi yanayojumisha hisabati ya juu ‘advance Mathematics’.

Tunafurahi wanafunzi hawa wanatoka kwenye shule mbalimbali wawili kati yao wanatoka kwenye shule za serikali shule ya sekondari za serikali,”amesema Prof. Mkenda.

Kati ya wanafunzi 50 , wanafunzi 16 wanatangulia Afrika Kusini kwenye Chuo Kikuu cha Johannesburg huku wanafunzi 34 watakwenda kwenye chuo kikuu cha Ireland.

Prof. Mkenda, amesema kuwa wanafunzi hao watanufaika kwenye masomo ya darasani lakini kipekee wapata uzoefu kwa kuunganishwa na kampuni za kiteknolojia zilizopo nchini huko “hii itawajengea uzoefu zaidi’’.

Amesema kuwa Wizara hiyo inatekeleza maagizo ya Rais Samia aliyoyatoa tarehe 14 Novemba 2025, alipokuwa anafungua bunge la 13 jijini Dodoma.

Rais Samia alisema kuwa aliiahidi kuwa serikali yake itawekeza kwenye sayansi ili kuzalisha wataalam katika teknolojia ya tehema, na atomiki.

Adhima yetu kuongeza wanasayansi wabebezi katika eneo la sayansi ya data, akili unde, sayansi ya kompyuta na teknlojia ya viwandani , tutatumia mfuko wa Samia Scholaship kuwasomesha wanasayansi kuwafanya wabebezi ndani na nje ya nchi,”.

Rais Samia ameelekeza wanafunzi wote wakaosoma shahada za sayansi kupata ufadhili wa serikali “tunafurahi serikali inaahidi na kutekeleza kwa wakati”

Prof. Mkenda, ameongeza kuwa “hata siku mia za tangu kuingia madarakani Rais Samia ahadi hii ameitekeleza”

Prof. Mkenda amesema kuwa serikali itaendelea kutoa ufadhili kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya sayansi ili kukidhi mahitaji katika maeneo mbalimbali .

Tumeanza kuwa na uhaba mkubwa wa Watanzania waliosoma Sayansi ya Nyuklia, tushaanza kupeleka wataalam kwenye shahad ya pili kwenye sayansi ya Nyuklia

Wanafunzi wote waomaliza kidato cha sita kwenye tahsusi ya Sayansi wote wasomeshwe na serikali katika vyuo vikuu,”

Prof. Mkenda, ametoa wito kwa wanafunzi wa shule za msingi, sekondari kuweka jitihada za makusudi kwenye kusoma masoma ya sayansi “kwenye hili hakuna ujanja ujanja haijalishi wewe mtoto wa nani , hakuna upendeleo ukifaulu vizuri tunaorodhesha wa kwanza mpaka bajeti itakapoisha watasomeshwa na serikali”.

Kwa upande wake Profesa, Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, ametoa msisitizo kwa wanafunzi hao kuwa hatua hiyo ni ushahidi kuwa serikali inatekeleza dhamira yake ya kuendeleza elimu.

Kuwepo kwenu hapa leo ni ushahidi wa wazi wa dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuwekeza kwenye sekta ya elimu hususan eneo la sayansi na teknolojia,”amesema Prof. Nombo.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi Dk. Amos Nungu, amesema kuwa ufadhili huo ni utachochea maendeleo ya Sayansi, Teknoloji hususan eneo la akili unde.

Tunatarajia mpango huu utaibua mtazamo mpya katika eneo la maendeleo ya sayansi nchini”

Malaika Frolence, mnufaika wa ufadhili huo amesema kuwa nafasi kusema kweli safari yetu ilikuwa ndefu kuanzia kidato cha sita sisi tumekuwa wanafunzi 50 wa kwanza kwenye matokeo ya kidato cha sita kisha tukaanda kwenye chuo kikuu cha Nelson Mandela ambapo tulikuwa tukiandaliwa .

Tumejengewa uweze na misingi katika mambo mengi pamoja na kupata maarifa ya kuijua duania, mafunzo ya kompyuta na pamoja na usimamizi wa fedha.

Malaika kwa niaba ya wenzake ameishukuru Serikali kwa kuwapa ufadhili huo na kwamba sasa wapo tayari kupeperusha bendera ya taifa katika nyanja ya taaluma “tunaamini tutakuwa bora, na sisi tutakuwa sehemu ya kutimiza malengo ya dira ya nchi yetu ya 2050.”

Naye Simon Asilwe mnufaika wa ufadhili huo amesema kuwa utayari wa serikali kwao ni kama deni ambalo malipo yake ni kurejesha matunda ya utaalamu watakaoupata kupitia ufadhili huo.

About The Author

error: Content is protected !!