Thadey Kweka
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limemwachia kwa dhamana Thadey Kweka ambaye ni raia wa Marekani mwenye asili ya Tanzania. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kweka alikuwa akishikiliwa tangu 8 Desemba 2025 katika kituo kikuu cha Polisi Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kuachiwa kwake leo 3 Januari 2026.
Taarifa za kukamatwa kwa Kweka zilitolewa 29 Desemba 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime baada ya kusambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba mwananchi huyo ambaye anaishi nchini Marekani alitekwa mkoani humo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda Maigwa imeeleza kuwa Kweka alikamatwa kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zikimkabili ikiwemo uchochezi.
ZINAZOFANANA
Meridianbet yachochea mwamko wa usafi wa mazingira Mbezi Juu
Kesi ya Mwambe yapigwa kalenda, kusikilizwa Januari 26
NBC yaahidi kuimarisha ushirikiano na wadau, yasisitiza mwelekeo wake