WAZIRI Mkuu Mwigulu Nchemba leo tarehe 29 Desemba 2025 amekagua hali za uzalishaji na usambazaji wa maji eneo la Ruvu Chini, mkoani Pwani. Anaripoti Zakia Nanga, Pwani … (endelea).
Akizungumza baada ya ukaguzi huo Mwigulu amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi, Serikali ilianza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
“Mipango hii ya ujenzi wa miradi inayolenga kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji ilianza muda mrefu, Serikali iliona na ilianza kutafuta majawabu ya hali hii miaka mitatu iliyopita kwa kujenga miradi mikubwa itakayotoa matokeo chanya,” amesema Mwigulu.
Naye WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) kwa kipindi ambacho kulikua na changamoto ya upatikanaji wa maji kutoa bili inayoendana na matumizi husika.
Aweso ameyasema hayo hii leo tarehe 29 Desemba 2025 wakati wa ukaguzi wa hali ya uzalishaji na usambazaji wa maji eneo la Ruvu chini mkoani Pwani ambapo amewataka Dawasa kutoka maofisini na kugawa maji.
“Dawasa hawana kisingizo mtoke ofisini tuna maji toshelevu,pelekeni maji kwa wananchi”alisema Aweso
ZINAZOFANANA
TMA yatangaza mvua kubwa zitakuja, mikoa 14 kuathirika
TRC yaomba radhi na kuongeza safari za SGR
Dk. Mohamed aendeleza mageuzi katika jamii ya Mtambwe