RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewaongoza waombolezaji kushiriki ibada ya mazishi ya mbunge wa Peramiho (CCM) Jenista Mhagama. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Ibada hiyo inafanyika hii leo tarehe 13 Desemba 2025 kwenye Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa kiwanja cha Ndege, jijini Dodoma.
Jenista ambaye alifariki tarehe 11 Desemba 2025, mwili wake utaagwa hii leo jijini humo na kisha kusafirishwa mpaka Peramiho mkoani Ruvuma ambapo mazishi yatafanyika Jumanne ya tarehe 16 Desemba 2025 kijiji cha Ruanda, Mbinga mkoani Ruvuma.
Mpaka umauti unamkuta Jenista alikuwa Mbunge wa jimbo la Peramiho ambalo amehudumu kwa miaka 20.
ZINAZOFANANA
Jiji kubwa, changamoto kubwa: Uhaba wa maji waitesa Dar
Uhusiano na ACT-Wazalendo, bado uko imara – Mpina
Dawasa yawapa matumaini wakazi wa Dar suala la maji