December 10, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Siku ya Uhuru, isiyokuwa huru

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita

 

CHAMA cha ACT -Wazalendo, kimesema kuwa Tanganyika imeazimisha sherehe za uhuru wake kukiwa hakuna uhuru kufuatia hatua zilizochukuliwa na dola kudhibiti uwezekano wa kutokea maandamano yaliyotangazwa na wanaharakati. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Jana tarehe 9 Desemba 2025, imetimia maika 64 ya uhuru wa Tanganyika ambapo mwaka 1961 taifa hilo lilitwa uhuru wake kutoka kwa wakoloni .

Ameyasema hayo leo tarehe 10 Desemba 2025 , makamu mwenyekiti wa ACT Wazalendo -Bara Isihaka Mchinjita ambapo amesema kuwa maandamano ya amani yalipangwa kote nchini ili kudai haki kwa waathiriwa wa ghasia baada ya uchaguzi na uwajibikaji kwa waliohusika.

Hata hivyo, Serikali ilipiga marufuku, ikituma vikosi vya usalama. Vitendo hivi vinathibitisha woga wa Serikali kwa sauti ya wananchi.

Aidha ACT, inasisitiza kuikataa tume ya uchunguzi wa ghasia baada ya uchaguzi chini ya Jaji Mkuu Mstaafu Othman Chande. Tunaiona Tume ya Chande kama udanganyifu mkubwa kwani inakosa Uhuru, Uwazi, na ushirikishwaji mpana wa jamii. Chombo hiki kilivyo hakiwezi kutoa haki kwa mamia waliouawa, maelfu waliokamatwa au kutoweka kwa kutekwa.

Pia ACT Wazalendo wamehimiza kuanza upya kwa mchakato wa katiba mpya ili kuunda mfumo unaohakikisha demokrasia ya kweli, ulinzi wa haki za watu na uwajibikaji

About The Author

error: Content is protected !!