December 8, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hakuna tishio la kuzima mtandao nchini – Simbachawene

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene

SIMBACHAWENE- HAKUNA TISHIO LA KUZIMA MTANDAO
WAZIRI wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, amesema uamuzi wa kuzima mtandao (internet) ni chaguo la mwisho kabisa pale hali ya kiusalama inapokuwa mbaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

KAULI hiyo ameitoa leo tarehe 8, Desemba 2025, kuwa hadi kufikia sasa hali ya Tanzania bado ipo shwari na hakuna tishio la kuiifanya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wazime mtandao kesho tarehe 9, Desemba 2025.

“Nyenzo kubwa inayotumika na hawa wanaharakati wa mitandaoni ni kutumia taarifa za taharuki, zikitoka wengine wanapata shida sana wakisikia, wengine wanazifurahia, kwa hiyo mpaka sasa hatujaona tishio lolote la kutufanya tuseme kwamba mtandao ndiyo tatizo.”

Pia amesema mtandao ndiyo hutumika katika utoaji wa huduma za kijamii nyingi kwenye benki, usafiri na huduma nyinginezo hivyo kuzima ni mwisho mambo yanapokuwa mabaya.

“Mimi naona kwakweli mpaka sasa hivi mambo si mabaya. Sisi ndiyo tunaangalia usalama wa raia na mali zao tunaona hali ni shwari, hakuna tishio kwamba wenzetu wa TCRA watazima mtandao.

About The Author

error: Content is protected !!