TANZANIA imeibuka kinara wa utalii duniani kama nchini inayoongoza kwa utalii wa safari katika tuzo zilizotolewa usiku wa jana tarehe 6 Desemba nchini Bahrain. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Tanzania imeshinda tuzo katika maeneo manne ikiwemo Visiwa vya Zanzibar kama eneo bora Afrika kwa mikutano na matukio ya kitaasisi, Hifadhi ya Serengeti kuwa hifadhi bora duniani, huku Kisiwa Thanda Resort moja ya visiwa vya Mafia kikiibuka kuwa kisiwa bora duniani cha mapumziko na tuzo ya kundi la sekta binafsi ikibebwa na kampuni ya Serengeti Balloon Safaris kama kampuni bora duniani ya safari za puto.
Tanzania imeendelea kushikilia nafasi yake ya kimataifa kama ‘nchi Inayoongoza duniani kwa utalii wa safari’ katika hafla ya fainali za World Travell Awads 2025.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hizo za WTA, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Hassan Abbai, amesema tuzo hizo ni uthibitisho wa kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya Tanzania pamoja na sekta binafsi katika kukuza utalii endelevu na kuimarisha uhifadhi nchini.
ZINAZOFANANA
Jaribio la Mapinduzi Benin lazimwa
Serikali ya Benin imepinduliwa
TRA yawataka wanachama wa SACCOS kuhamasisha ulipaji kodi