FILE - Benin's President Patrice Talon attends a meeting with Brazilian President Luiz Inacio Lula da Silva at Planalto presidential palace in Brasilia, Brazil, on May 23, 2024. (AP Photo/Eraldo Peres, File)
JARIBIO la mapinduzi linaendelea nchini Benin, baada ya kundi la wanajeshi kudai kwamba wamemwondoa Rais Patrice Talon madarakani na sasa wanachukua usimamizi wa nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Wanajeshi hao, waliounda kile walichokiita “Kamati ya kijeshi”, walionekana kwenye runinga ya taifa Jumapili asubuhi wakitangaza kwamba wamesitisha katiba, kuvunja serikali na kufuta shughuli za vyama vya siasa.
Jaribio hilo la mapinduzi linatokana na kundi la wanajeshi kudai kutoridhishwa na namna Rais Talon alivyokuwa akiiongoza nchi.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani, kundi hilo linaongozwa na Luteni Kanali Pascal Tigri.
Hadi sasa haijafahamika Rais Talon alipo, kwani wanajeshi wameripotiwa kufika katika makazi yake mjini Cotonou. Hata hivyo, shirika la habari la AFP limemnukuu msemaji wa Ikulu likisema kuwa rais yuko salama na jeshi linaanza kurejesha udhibiti.
Milio ya risasi ilisikiwa asubuhi katika mji huo, huku taarifa zikisema helikopta za kijeshi zilikuwa zikizunguka angani juu ya Cotonou.
Ubalozi wa Ufaransa umewataka raia wake kubaki majumbani kwa ajili ya usalama wao.
Benin inatarajiwa kufanya uchaguzi wa urais Aprili 2026, ambao ndiyo mwisho wa muhula wa Rais Talon. Ameshathibitisha kutogombea muhula wa tatu na tayari amemtaja mrithi anayemtaka.
Jaribio hili la mapinduzi nchini Benin limekuja siku chache tu baada ya Rais Umaro Sissoco Embaló kupinduliwa katika nchi jirani ya Guinea-Bissau.
Katika miaka ya karibuni, Afrika Magharibi imekumbwa na misururu ya mapinduzi, hali inayoongeza hofu ya kuzorota kwa usalama wa eneo hilo.
ZINAZOFANANA
Jaribio la Mapinduzi Benin lazimwa
Tanzania yaibuka kinara wa utalii duniani
TRA yawataka wanachama wa SACCOS kuhamasisha ulipaji kodi