December 5, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Uwezekano wa wanawake kuwa Mashemasi bado mgumu

Papa Leo XIV

 

TUME ya Juu ya Vatican imeendelea kupinga uwezekano wa kuruhusu wanawake wa Kikatoliki kuhudumu kama mashemasi ndani ya kanisa hilo ulimwenguni. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Tume hiyo ambayo imeasisiwa na Papa Leo XIV imeendeleza mchakato ulioasisiwa na watangulizi wake kuhusu kupendekeza wanawake kuhudumu katika nafasi ya mashemasi ilipiga kura na kuamua kupinga mapendekezo hayo.

Katika ripoti ya tume hiyo kura 7-1, zimesema utafiti wa kihistoria na uchunguzi wa kitheolojia haujumuishi uwezekano wa kuruhusu wanawake kuhudumu kama mashemasi kwa wakati huu lakini imependekeza utafiti zaidi wa suala hilo.

Ripoti hiyo imesema tathmini ya kundi hilo kuhusu suala hilo ilikuwa na nguvu, lakini hadi leo haijaruhusu uamuzi mahususi kutekelezwa.

Marehemu Papa Francis alianzisha tume mbili za kuchunguza uwezekano wa wanawake kutumikia kama mashemasi wa Kikatoliki, lakini alitoa angalizo kuwa hawawezi kuadhimisha misa.

Ripoti hiyo ya ni mara ya kwanza matokeo ya majadiliano hayo kuwekwa hadharani.

Papa John Paul II aliwahi kupiga marufuku wanawake kuhudumu kama mapadri mwaka wa 1994, lakini hakuzungumzia hasa suala la mashemasi wanawake.

Wanaotetea suala hilo wanaonyesha ushahidi kwamba wanawake walitumika kama mashemasi katika karne za mwanzo za Kanisa.

Mwanamke mmoja, Phoebe, anatajwa kuwa shemasi katika mojawapo ya barua za Mtume Mtakatifu Paulo.

About The Author

error: Content is protected !!