RIDHIWANI Jakaya Kikwete, waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, amesema yupo tayari kuhojiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, juu ya tuhuma ya mali alinazomiliki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na watumishi wa wizara hiyo, 26 Novemba 2025, Ridhiwani alisema, ni vyema taarifa za watumishi wa umma wakawa waadilifu kwa kuwa wananchi waliowengi wanachukizwa na kutokuwapo uadilifu kwa viongozi wa umma.
zikawa wazi na pale panapokuwa na walakini, ili waweze kuhojiwa na taarifa ziwekwe hadharani ili umma uwe na taarifa sahihi. “malalamiko juu ya viongozi yamekuwa mengi sana haijulikani lipi ni kweli lipi si kweli”
“…kwa mfano, maandamano yaliyotokea juzi hapa, malalamiko yalikuwepo makubwa juu ya maadili ya viongozi …kuna mtu mmoja anaitwa Ali Edha ana vituo vyake vya mafuta, vinaitwa Lake Oil, vingi vimechomwa moto kwa sababu zinasemwa ni za Ridhiwani.”
Akaongeza, “Malalamiko juu ya viongozi yamekuwa mengi sana, haijulikani lipi ni kweli lipi si kweli. Fanyeni kazi. Waiteni kuwahoji na mkimaliza, iteni waandishi wa habari na kuwaeleza mlichokifanya.”
Amesema, ni wajibu wa tume hiyo kumuita mtu yoyote bila hofu ili kumhoji; ni vema kukafanyika uchunguzi kwanza kabla ya kuita wahusika.
“Mkimaliza kuwahoji viongozi wa umma, muite mkutano na waandishi wa habari na muombe ushahidi mwingine wa ziada kwa umma, ili mueleze kilichofanyika,” alifafanua.
Katika maandamano hayo yaliyofanyika 29 Oktoba, kupinga kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, waandamanaji walichoma moto vituo kadhaa vya mafuta vya Lake Oil na kuharibu miundo yake mengine.
Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa wakati wa maandamano hayo ya siku tatu ya uchaguzi, huku chama kikuu cha upinzani nchini (Chadema) kikisema, takribani watu 700 wameuawa na vikosi vya usalama.
Mpaka sasa, serikali imekataa kutaja idadi kamili ya watu waliouawa kwenye ghasia hizo.
ZINAZOFANANA
Buckreef Gold yaimarisha ushirikiano na jamii, yapitia upya makubaliano yao
Jaji Mkuu kuziamua kesi za uchaguzi Zbar
Njama za kumlipa Singasinga zafichuka