Rais wa TLS, Boniface Mwabukusi
BONICFACE Mwabukusi, Rais wa chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), amesema vitisho kwa mawakili waliojitoa kusaidia wananchi katika kuwapatia msaada wa kisheria ni sawa na kubaka na kunajisi Mfumo wa utoaji haki na Mfumo wa haki jinai. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Ameyasema hayo leo tarehe 27 Novemba 2025, kupitia ukurasa wake wa ‘X’ zamani Twitter na kusema tulipofikishwa hatuwezi kutoka na propanganda kuwa tunaonewa wivu au raslimali chache au nyingi au uzalendo.
“Narudia tena. Hapa tulipofikishwa na utepetevu wa vyombo vya maamuzi pamoja kwa kuharibu demokrasia, uwajibikaji na Utawala wa sheria hatuwezi kutoka kwa Propaganda za tunaonewa wivu? Sijui tuna raslimali chache au nyingi au sijui uzalendo! au sijui dada yule anayeishi nje au huyu anayeishi ndani wanatumika na mabeberu!?
Mwabukusi amedai kuwa chanzo cha sintofahamu kinajulikana ni kuvuruga demokrasia nchini na kusababisha vijana kupoteza Tumaini, na kusema kazi hii ilisimamiwa na wao wenyewe kupitia vyombo vyao kwa kujua au kutokujua au kutokujali kwamba wakijikita hapo watapata majibu.
Pia amesema vijana wa GenZ wana akili kuliko wao na wamebeba maono bora ya Taifa kuliko wale wanaojiangalia wenyewe na wanajua wanapotaka Taifa lao lielekee kwakuwa wao sio “wagonga meza wazee wa ndio”
Amemalizia kwa kusema bado hatutaki kujifunza kwa uzembe uliopelekea mauaji na vifo vya wengi wasiokuwa na hatia kufuatia vurugu za uchaguzi na badala ya uchambuzi wa kitaalamu “tunapiga ramli chonganishi”
ZINAZOFANANA
Waziri Kikwete akutana na watumishi wa e-GA
Maswali tata ya Wahariri kwa Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba
Vyombo vya habari vimesifiwa au vimedhihakiwa?