SSI. Paul John Mselle
IDARA ya Uhamiaji imekanusha taarifa zinazosambazwa kupitia klipu ya sauti kwenye mitandao ya kijamii zikidai kwamba raia wa Tanzania wanaorejea nchini kutoka nje wananyang’anywa pasipoti na fedha zao katika viwanja vya ndege au vituo vya kuingilia nchini, kisha kuelekezwa kwenda kuhojiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tanzania, Dodoma. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumatatu tarehe 10 Novemba 2025 na msemaji wa Idara hiyo SSI. Paul John Mselle imeelezwa kuwa madai hayo ni ya uzushi na yamelenga kupotosha umma pamoja na kuleta taharuki katika jamii.
Idara ya Uhamiaji imewahakikishia Watanzania kuwa huduma zote kwa wananchi na wageni zinaendelea kutolewa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.
Vilevile, imewataka wananchi kupuuza taarifa zisizo rasmi na kutegemea vyanzo sahihi vya Serikali kwa taarifa za uhakika.
Miongoni mwa viongozi wa kisiasa waliowahi kuripoti kunyang’anywa pasipoti zao ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche,Godbless Lema na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi CHADEME Brenda Rupia
ZINAZOFANANA
Rais Mwinyi asisitiza Serikali ya Umoja wa Kitaifa
Serikali yaweka pingamizi kesi ya Heche dhidi ya IGP
Kesi ya Lissu yaahirishwa kwa sababu za kiusalama