November 6, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Watu 300 waliokamatwa kwenye maandamano Kilimanjaro waachiwa

SACP Saimon Maigwa

 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Saimon Maigwa, amesema watuhumiwa 300 waliokamatwa kwenye maandamano waliokamatwa awali wameachiwa baada ya kubainika hawakuwa na makosa. Anaripoti Joyce Ndeki, Kilimanjaro … (endelea).

Kuanzia tarehe 29 Oktoba maeneo mbalimbali nchini kuliripotiwa maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga kufanyika kwa uchaguzi Mkuu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, jana tarehe 5 Novemba 2025, Kamanda Maigwa alifafanua kuwa hadi sasa hakuna ripoti yoyote ya mauaji au majeruhi kwa raia au askari Mkoani humo kufuatia vurugu zilizoripotiwa wakati wa kipindi cha uchaguzi, na amesema kuwa hali ya usalama katika mkoa huo imerejea kuwa shwari na Jeshi la Polisi linaendelea kufanya doria kuhakikisha amani inaendelea kudumu.

Pia amekiri kuwa watu 11 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuchochea vurugu, ambapo 9 wanaoshikiliwa kwa kuchoma matairi na wengine wawili wanashikiliwa kwa kuhamasisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii.

Aidha, alikanusha taarifa zilizoenea mitandaoni zikidai kuwapo kwa vifo vilivyotokana na maandamano katika mamlaka ya Mji mdogo wa Himo, akisisitiza kuwa taarifa hizo si za kweli.

About The Author

error: Content is protected !!