November 5, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Wabunge wateule waitwa Bungeni Dodoma

Ado Shaibu, Mbunge mteule wa Tunduru Kaskazini

 

WABUNGE wateule wote wanafahamishwa kwamba shughuli za usajili na taratibu nyingine za kiutawala zitafanyika Ofisi ya Bunge Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 10 Novemba 2025, taarifa hiyo imetolewa na katibu wa bunge Baraka Leonard hii leo tarehe 5 Novemba 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kufuatia Tangazo la Rais la kuitisha Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la Serikali,toleo Maalum Na. 11 (Special Supplement) la tarehe 4 Novemba, 2025 Tangazo Na. 647A.Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 13 kitafanyika tarehe 11
Novemba, 2025 kama ilivyotamkwa kwenye Tangazo la Rais; na shughuli zitakazofanyika katika Mkutano huo ni pamoja na:

(a) Kusomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge
(b) Uchaguzi wa Spika
c) Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wote
(d) Kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu
(e) Uchaguzi wa Naibu Spika; na
(f) Ufunguzi rasmi wa Bunge Jipya utakaofanywa na [10:20, 05/11/2025] Boss Salehe: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Utaratibu wa uchaguzi utakaotumika kujaza nafasi ya Spika na Naibu Spike umetangazwa katika Tangazo Na. 14824A na Na. 14824B kwenye Gazeti la Serikali Toleo Maalum Na. 11 (Special Supplement) la tarehe 4 Novemba, 2025.

Aidha, inasisitizwa kwamba Wabunge Wateule wote wafike wakiwa wamevae mavazi rasmi kwa ajli ya zoezi la usaili na upigaji picha pamoja na nyaraka
zifuatazo:
(a) Hati ya Kuchaguliwa/Kuteuliwa kwa Mbunge
(D) Kitambulisho cha Taifa na nakala yake:
(c) Kadi ya Benki yenye Namba ya Akaunti ya Mbunge
d) Cheti halisi cha Ndoa kinachotambuliwa na Serikali (kwa wenye Ndoa) na nakala yake.
(e) Vyeti halisi vya kuzaliwa vya watoto wenye umri chini ya miaka 21 (kwa wenye watoto/wasiozidi wanne) na nakala Vyeti halisi vya Elimu/Taaluma vyenye ithibati ya taasisi husika na nakala zake;
(g) Wasifu wa Mbunge (Curriculum Vitae).

About The Author

error: Content is protected !!