October 25, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hatuna mawakala, kura zitalindwa na INEC

ZIKIWA zimebaki siku nne kufikia siku ya kupiga kura tarehe 29 Oktoba kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani , baadhi ya vyama vya siasa vimesema kuwa havina uwezo wa kuweka mawakala wa kusimamia kura zao hivyo jukumu hilo wanaiachia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), kusimamia na kulinda kura zao. Anaripori Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Wakuli AAFP, UPDP, na NRA.

Rajab Hoza, Naibu Katibu Mkuu wa UPDP, amesema kuwa chama hicho hatamudu gharama za kuweka mawakala nchi nzima hivyo wao wanaamini INEC itawalindia kura zao.

“Mawakala katika nchi nzima ukiweka ni hela nyingi sana hata kila wakala ukimpa shilingi 10 Elfu, kwa sababu huwezi kumweka wakala kituoni asubuhi mpaka jioni bila kumpa hela ya kula”

“Sasa kwa sisi UPDP wakala wetu atakuwa Tume ya Uchaguzi atulindie kura zetu uwezo wa kuwalipa mawakala hatuna hivyo tumeamua wakala wetu awe tume ya uchaguzi,”amesema Hoza.

Kwa upande wake mgombea urais kwa tiketi ya chama cha NRA, Almas Kasabya, amesema kuwa chama hicho hakitaweza kuwalipa mawakala na kwamba chama hicho kinaamini hakitaibiwa kura zake .

“Mawakala wanatakiwa walipwe lakini taasisi zetu ni ndogo haziwezi kuwalipa mawakala nchi nzima katia vituo zaidi ya elfu 97 tunaweza tusipate wote lakini tunaamimi Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu zilizowekwa ni ngumu sana mtu kukuibia kura,”.

“Tunaamimi maeneo ambayo hatutaweka mawakala kura zetu zitahesabiwa na zitakuwa salama,”amesema Kasabya.

Rashid Rai, Katibu Mkuu Chama cha Wakulima amesema kuwa chama hicho hakitakuwa na uwezo wa kuweka mawakala nchi nzima kwa hiyo wagombea ubunge na udiwani wataweka mawakala katika maeneo yao.

Bakari Makame , Naibu Katibu wa Uenezi wa TLP amesema kuwa chama chao kimemudu kuweka mawakala.

About The Author

error: Content is protected !!