SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kwa umma kuhusu ajali iliyohusisha treni ya EMU iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Dodoma majira ya saa 2:00 asubuhi. Anaripoti Zakia Nanga, Pwani … (endelea).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ajali imetokana na hitilafu za kiutendaji ambazo zilisababisha mabehewa matatu ya treni hiyo kuacha njia katika kituo cha Ruvu. TRC imethibitisha kuwa hakuna tukio lolote la vifo lililoripotiwa kufikia sasa.
Timu ya wataalamu ikiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TRC, vyombo vya ulinzi na usalama na menejimenti ya shirika hilo, inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha ajali hiyo.
TRC imewahakikishia wananchi kuwa juhudi zinaendelea kuhakikisha huduma za reli zinarejea haraka.
Shirika hilo pia limeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kufuatia tukio hilo.
ZINAZOFANANA
TMA yatangaza mvua kubwa zitakuja, mikoa 14 kuathirika
TRC yaomba radhi na kuongeza safari za SGR
Mwigulu akagua uzalishaji na usambazaji maji Ruvu chini