
Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema akiwa mahakamani
MAHAKAMA Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imekubali pingamizi la Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeshtakiwa katika mahakama hiyo kwa tuhuma za uhaini. Lissu alipinga mahakama hiyo kupokea ripoti ya Shahidi wa tatu wa serikali Samweli Kaaya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kesi hiyo inayosikilizwa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Iringa, Dunstan Ndunguru, akishirikiana na majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde katika hatua ya ushahidi wa Jamhuri, ikiwa ni shahidi wa tatu.
Akitoa uamuzi huo leo tarehe 23 Oktoba 2025, Jaji Kiwonde amesema kuwa licha kuwa shahidi huyo kuwa ni mtaalamu lakini alipwasa kuandaa Certificate.
“Kwetu sisi tunaona kazi yake ni kuzichunguza zile picha na baada ya kufanya huo uchunguzi yeye analo jukumu la kuandaa certificate,” alisema Jaji Kiwonde.
“Tunakubaliana na Mshitakiwa kuwa shahidi alipaswa kuandaa Certificate badala ya kuandaa ripoti, kwenye kesi hii shahidi namba tatu aliteuliwa kushughulikia picha mnato ambazo zinapelekwa kwake na hilo tulisema jana pia na mwishoni anaandaa certificate.
ZINAZOFANANA
SGR yasimamisha safari zake
TRC yataja chnzo cha ajali ya treni ya SGR Ruvu
Lissu aweka pingamizi lingine, mahakama kutoa uamuzi kesho.