Tundu Lissu akiwa mahakamani
TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeshtakiwa kwa uhaini katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, amemuuliza maswali ya dodoso shahidi wa pili wa serikali (John Kaaya) alimuuliza kama angewezekana mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo Luhaga Mpina apate haki kwenye mahakama ambayo majaji ni wateule wa rais na ndio mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), shahidi huyo akajibu isingewezekana.
Lissu: Uchaguzi wa mwaka huu mgombea urais wa ACT-Wazalendo ameenguliwa na Tume ya Uchaguzi?
Kaaya: Hajakidhi vigezo.
Lissu: Kaenguliwa na tume au hajaenguliwa?
Kaaya: Kaenguliwa na tume kweli.
Lissu: Je, Mwenyekiti wa Tume na Majaji waliokataa kesi jana wote si wateuliwa wa Rais?
Kaaya: Ni kweli.
Lissu: Sasa ulitegemea Mpina apate haki kutoka wapi kama wote aliokuwa anategemea wampe haki ni wateule wa Rais?
Kaaya: Ingekuwa ngumu sana kiukweli.
ZINAZOFANANA
Watu 172 kortini kwa kufanya vurugu, unyang’anyi siku ya Uchaguzi
Gwajima vigogo Chadema wasakwa na Polisi
Niffer, GEN Z washtakiwa kwa uhaini