
Humphrey Polepole
WAKILI wa Serikali Mwandamizi Faraja Nguka ameieleza Mahakama kuwa maombi yaliyofunguliwa na Familia ya Humphrey Polepole dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake wanne (4) wakitaka afikishwe mahakamani, hayatekelezeki kwa kuwa kiapo kilichowasilishwa Mahakamani hapo na Wakili wa mleta maombi (Peter Kibatala) hakijaonesha wazi ni nani hasa ambaye amemshikilia Polepole. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Aidha Wakili amesema kusema kuwa kupitia kiapo hicho Wakili anakili kwamba mteja wake amechukuliwa na watu wasiojulikana, na kwamba hadi sasa haijulikani alipo.
Sambamba na hilo Wakili wa Serikali ameieleza Mahakama kuwa, kupitia kiapo cha hicho, Wakili Peter Kibatala amedai kuwa ana mashaka kwamba mleta maombi anashikiliwa na mjibu maombi namba tano (5) katika kesi hiyo ambaye ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZPC) Faustine Mafwele.
Wakili Peter Kibatala akijibu hoja hizi amesema katika kiapo chake amebainisha wazi kwamba wajibu maombi wote ambao kwa ujumla wao wanawakilisha Jamhuri wanapaswa kumleta Humphrey Polepole Mahakamani, lakini amesema kuwa ombi hilo mahsusi linamuhusu mjibu maombi wa tano ambaye ni ZPC Mafwele.
Amesema amelazimika kuweka umahususi kwa Mafwele kufuatia taarifa za awali alizozipata kutoka kwa ndugu wa Humphrey Polepole, akiwemo Godfrey na Augusto Polepole ambao taarifa zao na madai yao zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo vya habari.
ZINAZOFANANA
Kitabu cha Lissu chazua gumzo mahakamani
Maswali ya majibu ya shahidi wa pili wa kesi ya Lissu
Kesi ya Polepole, IGP na wenzake wapewa siku tano kuwasilisha viapo