Peter Kibatala
WAKILI wa Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, Peter Kibatala amesema kuwa mahakama imewataka wajibu maombi ambao ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IJP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa upelelezi Kanda ya Dar es Salaam (ZCO) na Kamanda wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam (ZPC) na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha viapo vyao ndani ya siku tano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika shauri Na.21514/2025 ya Polepole dhidi ya Inspekta Jenarali wa Polisi na wenzake wannne ilifunguliwa tarehe 8 Oktoba 2025 katika Mahakama Kuu.
Viapo hivyo vinatakiwa kuwasilishwa mahakamani hapo tarehe 14 Oktoba 2025, huku maombi hayo yakitarajiwa kusikilizwa tarehe 15 Oktoba 2025.
ZINAZOFANANA
Watahiniwa 937,581 wafaulu elimu ya msingi
Mwabukusi alaani Heche kutuhumiwa kwa ugaidi
Rais Samia amuapisha Mwanasheria Mkuu