October 9, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Hivi ndivyo alivyohitimisha shahidi wa kwanza kesi ya Lissu

 

MAHAKAMA Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam inaendelea na kusikiliza shauri Na. 19605/2025 ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu – Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo leo shahidi wa awali wa serikali ASP George Bagyemu – Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, amehitimisha kutoa ushahidi wake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Leo tarehe 9 Oktoba 2025, Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga alimpitisha shahidi huyo kwenye maswali aliyoulizwa na Lissu ili kusawazisha, fuatilia kama ifuatavyo;-

Kabla shauri halijaendelea Lissu analalamikia utaratibu wa kuzuia ndugu zake kuingia mahakamano “ndugu zangu niliowaandika na kuwaomba waje hawajaruhusiwa kuingia inaonekana kuna mamlaka makubwa zaidi ya kuzuia nani aingie na nani asiingie”.

Jaji Dunstan Ndunguru anayeongoza jopo hilo anasema naomba tuendelee na hilo nitalitolea ufafanuzi baadae kidogo.

Wakati huo huo akasimama Katuga kwa ajili ya kuendelea kumsaili shahidi wake

Katuga: Sasa shahidi nikupe pole kwa yaliyokukuta kwa siku tatu.Tutauliza maswali yaliyo kwenye hati ya mashtaka.Uliulizwa kuhusu kufanya uchochezi ni uhaini sasa tuelezee hapa kufanya uchochezi ni uhaini?

Bagyemu: Anajibu: Kufanya uchochezi kwa nia ya kuitisha serikali ni uhaini.

Katuga: uliulizwa pia kuzuia uchaguzi ni kosa ukatujibu kuzuia kwa njia halali sio kosa elezea majaji ni kivipi?

Bagyemu: Kwenda mahakamani kuandika petition kuzuia uchaguzi sio kosa ila kuzuia uchaguzi kwa vitisho ni kosa la uhaini.

Katuga: Sasa shahidi tufafanulie kwa mujibu wa maelezo ya P nani alichapisha maneno hayo ukasema ni Tundu Lissu ukaulizwa pia mimi nina password za jambo TV ukasema sio mara ya mwisho ukaulizwa nani aliechapisha ukasema ni Lissu na shahid P sasa fafanua ulimaanisha nini?

Bagyemu: Mwenyekiti wa CDM Kwa kuongea na waandishi wa habari wewe ulichapisha

Katuga: Pia eneo hilohilo ukaulizwa ni nani aliepeleka maneno mtandaoni ukasema sio mtu wa jambo tufafanulie hayo maneno?

Bagyemu: Anasema nilimaanisha mtu wa jambo ni mwandishi wa habari ambae Lissu aliongea nae kwa malengo hayo maandishi yachapishwe mtandaoni.

Katuga: Kuna swali hapa ulianza na kupewa somo kuwa hii ni nchi ya kidemokrasia ukaenda mbele ukaelezwa kuwa kuipinga serikali ni kosa la uhaini ukajibu kwa njia halali sio kosa wafafanulie waelewe kwa njia halali inaruhusiwaje?

Bagyemu: Kama nilivoelezea kwenye maelezo ya halali kukosoa sio kosa ni vitisho kwa serikali watu wanaguna kidogo.

Katuga: For the purpose (kwa madhumuni) ya maswali yanayohusu mashtaka sisi tunaishia hapa.

Shahidi wa kwanza amemaliza kutoa ushahidi wake fuatilia MwanaHALISI Online kwa muendelezo wa mashahidi wanaofuata…

About The Author

error: Content is protected !!