October 7, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Yanayojiri kwenye kesi ya Lissu leo tarehe 7 Oktoba 2025, Mahakama Kuu

 

MAHAKAMA Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam inaendelea kusikiliza Kesi Na. 19605/2025 ya uhaini inayomakabili Tundu Lissu – Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo leo shahidi wa kwanza wa Jamhuri ASP George Bagyemu – Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam aliyetao ushahidi wake jana tarehe 6 Oktoba leo tarehe 7 Oktoba 2025, ni zamu ya upande wa utetezi ambapo Lissu anajitetea mwenyewe kumuuliza maswali ya dodoso (Cross Examination).

Katika maswali ya Lissu aliyomuuliza Bagyemu alimuuliza juu ya kifungu cha 39 (2) (b) ambapo kuna mchuano mkali wa maswali unaendelea.

Dodoso la maswali ya Lissu na Majibu shahidi ASP Bagyemu kama ifuatavyo;

Lissu: Jina lako ni George

Bagyemu : Ni jina langu.

Lissu: Sasa nakuuliza maswali nataka ndio au hapana.Nikisema toa maelezo toa, sitaki rongorongo.
Bagyemu : Sawa.
Lissu. Wambie majaji kama uliandika maelezo huko nyuma.

Bagyemu : Ndio niliandika.

Lissu : Ni kweli au si kweli uliandika maelezo mara mbili. Tarehe 8 na 10 Aprili 2025.

Bagyemu : Niliandika mara moja aaaaaa ni kweli niliandika mara mbili.

Lissu : Waeleze kama ukionyeshwe hayo maelezo yako utayatambua?

Bagyemu: Nikionyeshwa nitayatambua.

Lissu : Na mimi ninayo. Sasa niliyo nayo ni copy (nakala). Waheshimiwa majaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo ya maandishi ya mkono wake nisitumie haya copy ya kwangu.

Mawakili wa Serikali: Wanatafuta hayo maelezo, wanafungua makabrasha yao hapa.

Lissu : Umeyapata eee?

Bagyemu: Nimeyapata.

Lissu. Sasa waeleze majaji hivyo ni vitu gani? anza na ya kwanza tafadhali.

Bagyemu: Ya kwanza ni karatasi ya maelezo yako kwangu SSP George.

Lissu : Hati ya maelezo yako? Sahihi ni yangu.

Bagyemu: Ya pili pia ni maelezo yangu ya Nyongeza ya tarehe 10.

Lissu : Je hayo maelezo yana sahihi na wamabie ni za kwako?

Bagyemu: Ni za kwangu sahihi zote.

Lissu : Waambie majaji kama ni za kwako kama uko tayari ziingie kama ushahidi wa vielelezo vya utetezi?

Bagyemu: Hii ya kwanza niliandika

Lissu : Umeelewa swali langu kweli?

Bagyemu: Niko tayari ziingie mahakamani kama sehemu ya ushahidi.

Lissu : Waheshimiwa Majaji naomba hizo nyaraka ziingie kama kielelezo E01.

Anasimama Wakili wa Serikali: Renatus Mkude :-Anasema Waheshimiwa Majaji naomba Wakili Igans Semboka aseme. Anasimama Wakili Semboka na kudai kuwa Lissu yupo nje ya msingi ya sheria ya ushahidi kifungu Na. 164 na 173.

Wakili Semboka amezitaja kesi ya Shadrack Sospter Mkaruka Mangangari vs Jamhuri Rufaa No. 233/2022 , Lilian Jesus vs Jamhuri shauri la rufaa Na. 151/2018 Mahakama ya Rufaa na Shauri la Mahakama ya rufaa ambalo la Ruchere Mwita vs Jamhuri shauri la rufaa Na. 348/2013.

“Waheshimiwa Majaji mashauri haya yote yalieleza utaratibu wa kuzingatia na naomba ninukuu”
Lissu anasimama na kudai kuwa yeye hana hizo nakala za hizo kesi “wanaaongea hizo kesi hawanipatii, wanasema ziko tanzlii mfungwa anafikaje huko”.

Majaji wakautaka upande wa Jamhuri kumpatia nakala za kesi walizozitaja mahakamani hapo huku wakitaka watoe kesi moja isomwe ili kuokoa muda .

Wakili Semboka amesimama na kuieleza mahakama kuwa ukurasa wa 26 kwenye kesi ya liliani Jesus inaeleza kuhusu hatua za kufuata kabla ya mahakama haijapokea kielelezo .

“Shauri la Jamhuri vs Mnawara Hamis na wenzake 9 la mwaka 2022. Tanzlii. Jaji Manyanda alisema zipo taratibu 8 za kuzingatia maamuzi ya maelekezo ya mahakama ya rufani. Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaona mshitakiwa hajazingatia vigezo,”.

Naye Nassoro Katuga Wakili wa serikali Mkuu amesimama na kupigia msumari hoja za mawakili wenzake na kueleza kuwa msimamo wa kisheria ni kwamba hakuwezi kutolewa mahakamani kielelezo bila kufuata taratibu za kisheria. Na kuitaja kesi ya Mwanjilisi na wenzake watatu kesi ya rufaa ya jinai Na.154/1994 ilitaja njia kuwasilisha kielelezo mahakamani.

Naye Lissu akijibu hoja hizo amedai kuwa kwa ametanguloia hatua tatu mbele atakuwa tayari kurejea nyuma kufuata utaratibu uliolekezwa na mahakama ya rufani. “Shahidi amesema yeye hana shida maelezo ni yake na yapokelewe mawakili wake hawataki kabisa yapokelewe…,”.

“Kifungu cha 131 cha sheria ya ushahidi kinasema ukifanya jambo na upande mwingine ukachukua hatua, Mawakili wa serikali wamepinga wakati nyaraka bado haijapokelewa na mimi nimewakubalia…hili jambo wao linawaathiri nini kama shahidi ni wa kwao na maelezo ni ya kwao, hakuna wanachoathirika,”alidai Lissu.

Wakati huo Wakili Katuga amesimama na kudai kuwa kifungu cha 131 cha sheria ya ushahidi kinazuia mawakili kurejea nyuma ikiwa tayari washakosea.

Baada ya mabishano hayo ya muda mfupi mahakama hiyo ikatoa uamuzi wa kutopokea nyaraka hiyo. Lissu anaendelea na dodoso lake

Lissu: Elimu yako ulisema jana. Ulisoma kozi ya kwanza Moshi mieizi 6?

Bagyemu: : Ni kweli.

Lissu : Na baada ya hiyo course ukafuzu na kupata cheti, ukaajiliwa kama Polisi Constable?

Bagyemu: Ni sahihi kabisa.

Lissu : Baada ya hapo ulienda kusomea Course ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi hapa Dar es Salaam.

Bagyemu: Ni kweli.

Lissu : Hayo mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa polisi yalichukua miezi mingapi?

George : Miezi 9.

Lissu : Na baada ya hiyo miezi 9 ulipata cheti?

Bagyemu: Kweli nilipata cheti.

Lissu : Ukapandishwa cheo pia?

Bagyemu: Kweli nilipandishwa cheo kuwa Assistant Inspecto of Police.

Lissu : Sasa shahidi baada ya mafunzo hayo ulienda kusoma course ya tatu, Gazette officers course ?

Bagyemu: : Ni sahihi kabisa, nilienda chuo cha Polisi Dar ni kweli.

Lissu : Na ulisoma kwa miezi 9.

Bagyemu: Kweli kabisa.

Lissu : Baada ya hapo hujawahi kusoma tena na kupata cheti hadi leo, kwa mujibu wa ushahidi wako?

Bagyemu : Nimesoma course nyingine ndogondogo.

Lissu : Sijakuuliza ndogo ndogo.

Bagyemu:: Nimesoma refresher course kwa mwezi mmoja.

Lissu: Chuo gani?

Bagyemu: Mwezi mmoja pale Kidatu. Nikapata cheti.

Lissu : Na Chuo gani kingine?

Bagyemu: Mubarak Police Academy kule Egypt miezi miwil kipo Cairo.

Lissu : Ukapata shahada gani?

Bagyemu: Nikapata vyeti viwili pale.

Lissu: Sasa naomba uwaeleze majaji kama kuna mafunzo mengine uliyohudhuria yaliyokupa kitu kingine zaidi ya Cheti? Nataka kujua mafunzo mengine uliyowahi kupata.

Bagyemu: Nina advance diploma ya uhasibu nilimaliza 2001, Post Graduate Diploma in finance Chuo cha Sauti.Pia nimesoma masters of Bussiness administration nilimalizia Kisii University nchini Kenya. Nikasoma Masters of Human Resource Management Chuo Kikuu huria cha Tanzania. Nikapata pia cheti. Na sasa nimeanza PHD.

Lissu : Ni sahihi nikisema kwamba kwa mujibu wa PGO za 2021 wewe ni Professionally qualified member of the Police Officer?

Bagyemu: Ni sahihi kabisa.

Lissu : Unatambulika kama ni professionally officer?

Bagyemu: Ni sahihi kabisa.

Lissu : Sasa naomba waeleze kama maelezo haya ya hiki kisomo umeyaweka kwenye hati yako ya maelezo ya mashahidi?

Bagyemu: Nimeweka elimu yangu ya Kipolisi tu.

Lissu: Naomba nikusomee maelezo yako ya Tarehe 8 Aprili umesema hivi kuhusiana na elimu yako. Mimi mtajwa nimeajiriwa na kufanya kazi mikoa mbalimbali (Lissu amemsomea maelezo yake kisha akamuuliza , “…Sasa katika niliyosoma kama kuna chochote kinahusiana na vyuo vya Polisi ulivyotaja jana?

Bagyemu: Hakuna kabisa hayo mambo niliyosema jana kuhusu vyuo vya Kipolisi na vyeti nilivyopata.

Lissu : Ieleze mahakama kama mafunzo yako mengine nje ya upolisi hayo madiploma ya uhasibu na mengine ya sauti kama yapo kwenye hati yako ya maelezo wambie kama yapo?

Bagyemu: Kwenye hiyo hati haipo ila jana nikiwa naulizwa nilisema.

Lissu : Ulitaja au hukutaja jana?

Bagyemu: Sikutaja haikuwa na umuhimu na jana sikuulizwa ndio maana sikutaja.

Lissu : Na hizo masters hukutaja pia?

Bagyemu: Ndio sikutaja kwasababu sikuulizwa ila leo umeniuliza ndio maana nimetaja.

Lissu : Twende kwenye ushahidi wako wa siku ya tarehe 4Aprili 2025, uliiambia mahakama kwamba uliletewa taarifa za video clip yenye uhaini na ASP John Kahaya?

Bagyemu: Ni kweli.

Lissu : Ulisema pia ASP John kahaya alikwambia aliona video clip kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV yenye kichwa cha habari uso kwa uso na Watanzani ni sahihi?

Bagyemu: Ni kweli heading ilikuwa inasomeka hivyo.

Lissu : Sasa waambie majaji kama maneno yako hayo yapo kwenye maelezo yako ya mashahidi?

Bagyemu: Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu.

Lissu : Ulisema kwamba baada ya kuambiwa hivyo ulimwambia ASP John Kahaya. Akuonyeshe hiyo video clip?

Bagyemu: Ni kweli ilikuwa hivyo.

Lissu : Pia jana ulisema kwamba ASP kahaya alikuonyesha sehemu sehemu?

George: Ni kweli alifanya hivyo kwa siku ya tarehe 4.

Lissu : Waeleze kama haya maneno alikuonyesha sehemu sehemu hakukuonyesha yote kama yapo kwenye hati yako ya maelezo.

Bagyemu : Sidhani kama ipo nadhani haitakuwepo. Haipo sawa.

Lissu : Mtu anayetoa maudhui ya uchochezi ni kosa la uhaini, kweli au si kweli?

Bagyemu: Naomba nitoe maelezo.

Lissu : Sitaki maelezo we jibu maudhui ya uchochezi ni kosa la uhaini au sio kosa la uhaini.

Bagyemu: Ni kweli ni kosa la uhaini.

Lissu : Sasa jana ulitaja kifungu cha uhaini ni 39?

Bagyemu: Ni kweli we anza kusoma kwenye execution..

Lissu : unasema?

Bagyemu: Samahani ni EXECUTIVE.

Lissu: Ningeshangaa na kisomo chako chote usijue Kiengereza?

Bagyemu: Nimekosea hapo.

Kifungu cha 39 (2) (a&b), Mtu yeyote ambaye, yumo katika ndani ya Jamhuri ya Muungano, akiwa ndani ya Jamhuri ya Muungano au popote, anajenga nia kusababisha au kuwezesha kusababishwa, au anajenga nia ya kuchochea, anashawishi, shauri au kuusia mtu yeyote au kikundi cha watu kusababisha au kuwezesha kusababishwa yoyote kati ya matendo au malengo yafuatayo, yaani:- (a) kifo, kumlemaza au kumjeruhi, au kufungwa au kumzuia, Rais; (b) kumwondoa Rais madarakani isivyo halali kutoka katika wadhifa wake wa Urais au kumwondolea ufahari, heshima na jina la Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Jamhuri ya Muungano;

Lissu : Je video uliyoisoma hayo maudhui ya uchochezi yanaingia kwenye 39(2)d?

Bagyemu : Ndio yanaingia.

Lissu: Naona kama vingine unaruka kwenye hicho kifungu, twende taratibu tutamaliza vyote, naomba nikusomee maneno nikiyoshitakiwa nayo. Maneno ya uhaini yanasema hivi wanasema kitu kimoja hapa wanasema hivi ‘msimamo huu unaashiria uasi ni kweli , ni kweli kwa sababu tunasema tunaenda kuzuia uchaguzi na tutavuruga na tutakinukisha .Swali langu Je haya niliyosoma yapo kwenye hati ya mashitaka?

Bagyemu: Hayo uliyosoma hayapo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online

About The Author

error: Content is protected !!