
Msemaji wa Polisi, DCP David Misime
JESHI la Polisi limesema kuwa linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ambaye alijitambulisha kuwa ni Ndugu wa Humphrey Polepole ili aweze kulipa Jeshi hilo ushirikiano na kutoa maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa kwamba Afisa wa Jeshi la Polisi alihusika kumteka Polepole. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa hiyo ya Polisi pia imesema kama lilivyotoa taarifa yake jana tarehe 6 Oktoba 2025, kwamba limeanza uchunguzi wa tuhuma zilizotolewa na Augustino Polepole kuwa, Ndugu yao Humphrey Polepole ametekwa na jalada la uchunguzi lilifunguliwa jana hiyohiyo.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 8 Oktoba 2025 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma, imenukuliwa ikieleza yafuatayo “Pamoja na kukusanya taarifa mbalimbali, Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili aweze kutupa ushirikiano na kutoa maelezo yake na uthibitisho wa shutuma alizotoa kwamba, Afisa wa Jeshi la Polisi alihusika katika tukio alilolitolea taarifa kupitia mitandao ya kijamii”
“Hii inaenda sambamba na kututhibitishia kuwa Humphrey Polepole alikuwa ni Mpangaji ama Mkazi wa nyumba aliyodai kuwa utekaji ulifanyika”
ZINAZOFANANA
Yanayojiri kwenye kesi ya Lissu leo tarehe 7 Oktoba 2025, Mahakama Kuu
Mawakili wa Polepole watoa tamko
Polisi yasisitiza kumtaka Polepole kwa mahojiano