
Tundu Lissu akiwa mahakamani
TUNDU Lissu ameendelea kumbana shahidi kwa maswali ya dodoso kulingana na ushahidi alioutoa jana tarehe 6 Aprili 2025 ambapo shahidi wa kwanza wa Jamhuri aliendelea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu: wakati unaongoza hiyo timu ulisema, tarehe 6 Aprili ulimtafuta Mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa?
Bagyemu: siwezi kukutajia ila nilipata namba ya kiongozi wa Jambo TV sikujua jina lake kama ndio Marwa.
Lissu: Huyu Kiongozi wa Jambo TV uliyemtafuta ulimuomba akupatie hiyo video clip halisi iliyochukuliwa kwenye mkutano?
Bagyemu: Ni kweli.
Lissu: Ni kweli huyo kiongozi alikwambia mfanyakazi yupo Dodoma?
Bagyemu: Ni kweli, alinipa namba ya simu pia ni kweli ya huyo mfanyakazi wake.
Lissu: Ni kweli namba hiyo ulimpa DCP Ng’anzi?
Bagyemu: Ni kweli nilifanya hivyo.
Lissu: Ni kweli Ng’anzi alimpatia Andrew Churu yule Polisi mwingine?
Bagyemu: Hilo sijui kwakweli.
Lissu: Ni kweli tar. 07/04 DCP Ng’anzi alisema amempata huyo aliyerekodi?
Bagyemu: Ndio ni sahihi kabisa.
Lissu: Na memory card nayo alikwambia imepatikana?
Bagyemu: Ni kweli aliniambia hivyo.
Lissu: Ni kweli DCP Ng’anzi alikwambia kwamba memory card na card reader yake vitaletwa siku hiyo hiyo na Andrew churu ofisini kwako?
Bagyemu: Ni sahihi kabisa.
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba siku ya tarehe 7 Aprili Andrew Churu alisafiri kutoka Dodoma hadi ofisini kwako na kufika usiku?
Bagyemu: Ni sahihi kabisa.
Lissu: Je alikuja na hizo card, na vitu vingine?
Bagyemu: Ni sahihi alikuja navyo na alikuja pia na hati ya makabidhiano.
Lissu: Acha kiherehere hiyo hati sijakuuliza.
Lissu: Je ulisoma maelezo ya P hiyo tarehe 07 ulivyoletewa.
Bagyemu: Ni kweli nilisoma.
Lissu: Kwa vile ulisoma, kweli au si kweli huyo P alisema ni yeye ndie alirekodi mkutano na ni yeye alirusha kwenye Jambo TV akaunti, anamtafutia maelezo ya huyo P na anamwambia ayasome.
Bagyemu: “kuwa mimi nakumbuka mkutano …” (kabla hajamalizia Wakili Katuga anasimama).
Wakili Katuga: Haya maelezo sio yakwake shahidi kwahiyo asiulizwe.
Lissu: Anajibu shahidi mwenyewe ndio kasema kuwa alipelekewa maelezo na huyo P akasoma, na maelezo hayo ndio yanasema nani alichapisha?
Jaji: Msomee wewe tafadhali.
Lissu: P anasema ni wao Jambo TV ndio walikuwa wanarusha. Na wao ndio walirekodi.
Lissu: Je mimi ndie niliesambaza na kuchapisha?
Bagyemu: Ndio ni wewe uliyechapisha.
Wakili wa Serikali Katuga amesimama na kuiomba mahakama waende mapumziko “Tunaomba twende kwenye health break tutaendelea”.
Lissu: Sawa twende maana huyu shahidi ili nimalizane nae nahitaji siku zingine kama mbili au tatu. Kwahiyo bado tuko nae sana. Siwezi kumuacha haraka.
Majaji wameahirisha shauri mpaka saa tisa mchana kwa ajili ya kuendelea na ushahidi, endelea kufuatilia MwanaHALISI Online….
Lissu: Katika ushahidi wako ulisema kwanini kwa ufahamu wako maneno niliyosema ni uhaini?
Bagyemu: Kweli nilisema.
Lissu: Ulisema lengo waisikie Watanzania na wasio Watanzania?
Bagyemu: Ndio nilisema hivyo.
Lissu: Kuita waandishi wa habari ni kosa la uhaini?
Bagyemu: itategemea?
Lissu: Soma kifungu cha 39(2) d ya Penal code, kama kuna mahali kinasema kuita waandishi ni kosa la uhaini? Inasema hivyo?
Bagyemu, anaanza kusoma, lissu amemwambia soma wewe kimya kimya unijibu.
Bagyemu: Hayo maneno hayapo kwenye hiki kifungu kuwa kuita waandishi wa habari ni uhaini, Hayajasemwa kwenye sheria.
Lissu: Je tarehe 8 au 10 kwenye maelezo yako kuna mahali ulisema kuwa mimi kuita waandishi wa habari ni uhaini?
Bagyemu: Ulisema una kiapo kwenye maelezo yangu niliandika.
Lissu: hayo sijakuuliza we sema kwenye maelezo yako kama uhaini ni kuita waandishi wa habari?
Bagyemu: Hilo hakuna sijaandika hivyo na sikusema hivyo.
Lissu: Katika kuonesha maneno yangu yalikuwa ya kihaini ni kutoa na kuchapisha taarifa hizo mtandaoni?
Bagyemu: Ni kweli nilisema.
Lissu: Hizi video kwa vile ziko mtandaoni je litakuwa ni kosa la cyber?
Bagyemu: Yes litakuwa hata kosa lingine.
Lissu: Kosa langu ni kutoa na kuchapisha hii kutoa ni uttering?
Bagyemu: Yes ndio kingereza chake.
Lissu: Soma kifungu cha 3 cha cyber crime Act (sheria ya makossa ya mtandaoni) kifungu cha 3 cha sheria hiyo sasa soma maana ya neno uttering?
Bagyemu, anapewa sheria aisome ili atuambie maana ya uttering
Lissu: Kama ipo sema ipo.
Bagyemu: Nimeona ipo inasema communication.
Lissu: Sasa communication sijashitakiwa nayo.
Bagyemu: Uttering haipo sawa.
Lissu: kifungu cha 39(2)d cha Penal Code soma hayo maneno na uwambie kuna mahali neno uttering limeandikwa kama halijaandikwa usitupotezee muda sema halipo.
Bagyemu: … neno uttering halipo kiukweli. Hakuna kabisa.
Lissu: Kifungu cha 39(2)d lengo la uhaini kionekane kwa maandishi in writing, publication or any overt act?
Bagyemu: Ni sahihi iko hivyo.
Lissu: Neno publish maana yake nini soma kifungu cha 3 cha cyber crime act ili tujue maana ya kupublish?
Bagyemu, anasoma hapa kwanza, Publishing means distributing, transmitting, disseminating, printing or offering for sale. Umemaliza?
Bagyemu: Naendelea kidogo.
Lissu: Swali langu sasa shahidi kwa maelezo yako mwenyewe aliyepeleka kwenye mtandao wa Jambo TV ni nani?
Bagyemu: Mfanyakazi wa Jambo Tv.
Lissu: Kwa mujibu wa ushahidi wako wewe na P aliyerusha maneno hayo ni P?
Bagyemu: Hapana, aliyerusha ni wewe Lissu na P.
Lissu: Kama nilichapisha mimi na P kwanini P hajashitakiwa?
“Tutafika tu mmezoea kuwasingizia watu kwa makesi ya uongo ila tutafika tu. waonyeshe majaji kuwa P alisema Lissu alitutoa nje ili tusisikie maneno fulani fulani.
“Anangalia kwenye maelezo uniambie kama P alisema Lissu alitutoa nje ili kuna maneno tusisikilize,” amedai Lissu.
Bagyemu, anasoma “walibaki wenyewe Chadema wakatutoa kuzungumza mambo yao”
Lissu: Kuna mahali kuna jina la Lissu.
Bagyemu: Halipo hilo jina, halipo jina la Lissu.
Lissu: Umesema mimi ndie niliyewaalika waandishi wa habari Ile tarehe 3 Aprili.
Bagyemu: Ndio ni wewe ndiye uliwaita.
Lissu: Je niliwaita kwa njia ya simu?
Bagyemu: Sijui uliwaita kwa njia ya simu.
Lissu: Je barua?
Bagyemu: Sijui kwa njia gani? Mimi sijui uliwaita kwa njia gani?
Lissu: Je nilitangaza magazetini?
Bagyemu: Sijui mimi ulifanyia wapi?
Lissu: Je wewe ni polisi wa aina gani ambae hujui mkutano ulifanyika wapi?
Bagyemu: Hukutualika.
Lissu: Hujui niliwaalikaje?
Bagyemu: Sijui njia uliyotumia kuwaalika.
Lissu: Je ulimuhoji katibu mkuu wa Chadema kuhusu utaratibu wa kualika waandishi?
Bagyemu: Sikumuhoji.
Lissu: Je Amani Gorugwa ulimuhoji?
Bagyemu: Sikumoji.
Lissu ;Ulimhoji Brenda Rupia ulimuhoji kuhusu utaratibu wa kuita waandishi?
Bagyemu: Nilimuita lakini hakuja.
Lissu kwahiyo ulimuhoji?
Bagyemu: Sikumuhoji.
Lissu: Hujui walialikwaje, Hujui nani aliwaalika? Ila unang’ang’ania ni Tundu Lissu ndio alialika.
Bagyemu: Mimi sijui kwakweli.
Lissu : Waeleze majaji kama mimi ni mmoja wapo wa wakurugenzi wa Jambo TV.
Bagyemu: sina uhakika na hilo.
Lissu : Je mimi ni mmoja wa waandishi wa habari wa Jambo Tv ?
Bagyemu : sina uhakika na hilo pia.
Lissu : Ni kweli au si kweli hizo video zilipatikana kwenye mtandao wa Jambo Tv?
Bagyemu: Ni kweli zilipatikana huko Jambo TV.
Lissu : Je unafahamu mimi nina password za mtandao wa Jambo TV uliwaambia hilo majaji?
Bagyemu: Siwezi kufahamu kama unazo.
Lissu : Kama inawezekana kitaalamu kwa mtu asiye na password kuingia na kuweka chochote?
Bagyemu: Sijui uliingiaje na uliwekaje hizo video.
Lissu : Ulisema hizo video zilikuwepo kwenye mitandao mingine?
Bagyemu: P ndio alisema.
Lissu : Je hukuwa na interest kujua umechapisha kwa mitandao mingine?
Bagyemu: Sikuwa na interest mimi.
Lissu : Waeleze majaji kama umesoma maelezo ya Mahamba.
Bagyemu: Mimi sikusoma.
Lissu : Kwahiyo kumbe hukusoma maelezo ya Amin Mahamba?
Bagyemu: Sikusoma ndio.
Lissu : Hizi video clip zilifanyiwa uchunguzi wa kitaalamu cyber forensic analysis?
Bagyemu: Ni kweli kabisa zilifanyiwa.
Lissu : Kahaya ndio alifanya kazi hiyo?
Bagyemu: Ni sahihi kabisa.
Lissu : Ni sahihi Kahaya alisema camera iliyotumika ni aina ya Sony
Bagyemu : Maelezo yake sikusoma na yeye ni shahidi atakuja kutoa.
Lissu : Na Kahaya alisema hayo maneno yakiwekwa mtandaoni na Jambo Tv?
Bagyemu: Mimi sikusoma maelezo yake.
Lissu : Waeleze Kama ulisoma maelezo ya Andrew Churu. Yule askari wa Dodoma.
Bagyemu: Ya Andrew Churu sikusoma, mimi nilisoma ya P.
Lissu : Maelezo yako uliandikiwa na nani?
Bagyemu: Niliandika Mwenyewe.
Lissu : Je kabla ya kuandika maelezo hayo uliomba ushauri wa kisheria wa mwanasheria yoyote?
Bagyemu: Sikuomba ushauri kokote.
Lissu : Naomba usome kifungu cha 11(4) cha CPA. Ulisema umeandika kifungu cha 11(3)?
Bagyemu: Ni kweli.
Lissu : Ni sahihi hicho kifungu hakiruhusu mtu kujiandikia mwenyewe?
Bagyemu: Kinaruhusu unaweza kujiandikisha. Kama nilivyoeleza hakuna kifungu kinachozuia na mimi ni Police officer nilijiandika mwenyewe.
Lissu : Nani aliyekuonya, Nani aliyekukanya? Section 10(3) of CPA.
Bagyemu: Ni Mimi mwenyewe ndio nilijikanya
Lissu : Nani alithibitisha pale chini baada ya maelezo yako?
Bagyemu: Ni mimi mweneyewe, nilijiandika, nikajikanya na kujithibitisha mwenyewe.
Lissu : Ulisema mimi nina kiapo cha JKT nilitoa kinyume na kiapo changu?
Bagyemu: Ni kweli nilisema hivyo.
Lissu : Je wewe umewahi kwenda JKT?
Bagyemu: Mimi sijawahi kwenda JKT.
Lissu : Nilikwenda JKT kambi gani?
Bagyemu: Mwaka 1989 ulianzia mafinga iringa na baadae ukaenda Itende Mbeya. Ulifuzu na kupewa cheti.
Lissu : Je ulikuwepo mwaka 1989?
Bagyemu: Sikuwepo.
Lissu : Je ulikuwepo Itende?
Bagyemu: Sikuwepo hata Itende ila wewe umegombea urais taarifa zako zinajulikana.
Lissu : Ulikiona cheti changu cha Itende?
George: Nimeona copy yako.
Lissu : Sasa waeleze Majaji kama hayo uliyosema yapo kwenye maelezo?
Bagyemu: Hayapo.
Lissu : Kama nilienda jeshini miaka 39 mimi ni mwanajeshi?
Bagyemu: Wewe ni askari wa akiba.
Lissu : Soma ibara ya 147(4) ‘mnakaa huko mnadanganyana hamjui mambo mnajifanya mnajua”.
Jaji anasema Mshitakiwa tafadhali.
Bagyemu, anasoma Katiba sasa Mwanajeshi maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa masharti ya muda au kudumu katika jeshi la polisi, lawananchi, au la magereza au polisi.
Lissu : Sasa waeleze majaji kama mimi nimeajiriwa kwa muda katika mojawapo ya hayo majeshi.
Bagyemu : Wewe umeajiriwa na JKT.
Lissu : Je kwenda JKT mwaka 1989 na 1990 je nilikuwa nimejajiriwa?
Bagyemu: Hukuwa umeajiriwa.
Lissu : nilivyomaliza nilikuwa nimeajiriwa?
Bagyemu: Hukuwa umeajiriwa.
Lissu : Kwenye Katiba kuna maneno askari wa akiba?
Bagyemu: Hayapo kabisa kwenye Katiba.
Lissu : Waeleze kama umewasilisha hati ya kiapo cha utii cha kwangu hapa mahakamani?
Bagyemu: Sijakiwasilisha mimi, sijaleta hapa.
Lissu : Je mtu yeyote aliyepitia JKT anakuwa mwanajeshi milele? Askari wa akiba anatambulika kikatiba?
Bagyemu: Anatambulika.
Lissu : Hawa maaskari wa akiba wana masharti na askari wengine?
Bagyemu:: Ndio.
Lissu : Je Kikwete ni mwanajeshi alikuwa?
Bagyemu::Ndio alikuwa mwanajeshi.
Lissu : Katiba inasema itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama cha siasa?
Bagyemu: Ni kweli.
Lissu : Sasa kuhusu Kikwete alikuwaje Mwenyekiti wa CCM?
Bagyemu: Hilo sijui.
Lissu : Je Kinana nae?
Bagyemu: Nae sijui.
Lissu : Yusuph Makamba nae aliyekuwa katibu mkuu wa CCM alikuwa mwanajeshi na alikuwaje kiongozi wa CCM?
Bagyemu:: Yeye alikuwa Mwanajeshi mstaafu.
Lissu : Ni kweli National Prosecution Act kunapokuwa na kosa lolote ambalo adhabu ni kifo DPP anapaswa kujurishwa?
Bagyemu: Ndio ni kweli inapaswa kuwa hivyo.
Lissu : Kati ya tarehe 4 na tarehe 8 wakati nakamatwa Mbinga kama ulitoa taarifa kwa DPP?
Bagyemu: : Mpaka tarehe 8 nilikuwa sijapeleka.
Lissu : Na kwenye maelezo yako pia hujasema jambo hilo?
Bagyemu: : Ndio sijasema.
Lissu : Waeleze majaji Sheria ya NPS (National Prosecution ), niliyoitaja DPP au mawakili wake ndio wenye mamlaka ya kuratibu makosa ya jinai?
Bagyemu: Ni sahihi.
Lissu : Je DPP aliratibu upelelezi ukiwa Chief investigator?
Bagyemu: Kwa siku ambazo mimi nilikuwa kiongozi wa upelelezi sikuwahi kumuona wakili kutoka kwa DPP, hawakusimamia au kuratibu huu upelelezi.
Amesimama Wakili wa Serikali Renatus Mkude anasema Mheshimiwa Jaji muda umeenda na wenzetu wa Magereza wanasema barabara ni mbovu kwahiyo tunaomba kuahirisha hadi kesho.
Majaji wamemuuliza Lissu anasemaje kuhusu ombi la Wakili Mkude akajibu kuwa mahakama iwakubalie “Waheshimiwa Majaji basi tuwakubalie na mimi niende nikale, huyu niko nae sana, bado nahitaji kuendelea nae,”.
Wakati huo majaji wakatoa onyo juu ya kitendo mawakili kushikana mashati kilichotokea jana tarehe kabla ya shauri hilo kuanza .
Shauri hilo limeahirishwa mpaka kesho tarehe 8 Oktoba saa tatu asubuhi ambapo Lissu ataendelea kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyo .
ZINAZOFANANA
Kutekwa Polepole, Mawakili wake wamshtaki IGP, AG, DPP, ZPC
Yanayojiri kwenye kesi ya Lissu leo tarehe 7 Oktoba 2025, Mahakama Kuu
Polisi watangaza kumtafuta ndugu yake Polepole