October 6, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Polisi yasisitiza kumtaka Polepole kwa mahojiano

Msemaji wa Polisi, DCP David Misime

 

PAMOJA na taarifa zinazosambaa mitandaoni zikifuatana na video mbalimbali zinadai kuwa usiku wa kuamkia leo aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole ametekwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana, bado Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa bado linamsubiri Mwanadiplomasia huyo kwa mahojiano. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea). 

Taarifa hiyo imelezwa kuwa Polepole ametakwa nyumbani kwake baada ya kuvungwa geti na mlango na sehemu mbalimbali huku ikitapakaa damu, ishara kwamba alijeruhiwa vibaya wakati wa tukio hilo.

Kutokana na taarifa hizo kumeibua taharuki kubwa miongoni mwa wananchi, huku wito ukitolewa kwa vyombo vya usalama kuchukua hatua za haraka ili kubaini ukweli na kuhakikisha usalama wa Polepole.

Wakati hayo yakiendelea mtandaoni jeshi la polisi limetoa taarifa kupitia msemaji wake, David Misime imesema kuwa jeshi hilo linaendelea kumsubiri Humphrey Polepole aripoti katika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Polepole alitumiwa barua ya wito uliomtaka kufika katika ofisi za DCI ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao ya kijamiilakini hadi leo hajatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa sheria.

Jeshi la Polisi limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa ,tayari Jeshi la Polisi limeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake.

About The Author

error: Content is protected !!