Peter Kibatala
MAWAKILI wa Balozi Mstaafu Humphrey Polepole wametoa taarifa kwa umma wakizitaka mamlaka za usalama nchini kutumia rasilimali na mbinu zote kuhakikisha usalama wake na kutoa taarifa kwa Watanzania na dunia nzima. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala, imeelezwa kuwa Polepole amehudumia taifa kwa muda mrefu katika nafasi mbalimbali za utumishi wa umma, hivyo ana haki ya kulindwa kisheria na kiusalama kama raia.
Aidha, mawakili hao wamesisitiza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya jambo hili, zikiwemo hatua wanazochukua kwa kushirikiana na watu na taasisi mbalimbali duniani kote.
Tamko hilo limekuja kufuatia taarifa zinazodai kutekwa kwa Polepole usiku wa kuamkia tarehe 6 Oktoba 2025, tukio lililosababisha taharuki kubwa kwa wananchi.
ZINAZOFANANA
Wavumbuzi Vijana wa Tanzania Waongoza Mapambano ya Tabianchi
Gwajima acharuka tena, akemea utekaji
Mahakama: Hakuna ushahidi Polepole anashikiliwa na IGP na wenzake