
TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameieleza Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam kuwa orodha ya watu 100 watakaohudhuria mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili aliyoombwa aiwasilishe hakufanyiwa kazi, kuhusu kikao kabla ya shauri na alichokiita kupangwa hukumu yake kabla ya shauri kusikilizwa. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu amedai hayo leo tarehe 6 Oktoba 2025, wakati shauri hilo likiwa linataka kuanza kusikilizwa “Nina mambo nataka yaingie kwenye rekodi ya mahakama kwanza tarehe 30 Septemba 2025, Naibu Msajili anaitwa L.B Lyakinana aliniandikia barua kwa kupitia Mkuu wa Gereza la Ukonga, barua hiyo ilinifikia tarehe 2 Oktoba 2025, alhamisi iliyopita,” amedai.
Lissu ameendelea; “Barua hiyo ilinielekeza kwamba niwasilishe mahakamani orodha ya watu 100 wa upande wangu ambao ningependelea wahudhurie kesi hii na pamoja na mengine ilielekeza hayo majina yamfikie siku ya tarehe 3 Oktoba, kabla ya saa 12 jioni, niliipata tarehe tarehe 2 na tarehe 3 majina yawe yamemfikia msajili na watu hao ni pamoja na mawakili, viongozi wa chama na ndugu zangu.”
Lissu amedai kuwa akiwa gerezani bila mawasiliano ya mawakili wake alipambana akaanidka majina hayo na yakamfikia msajili huyo kwa muda alitakiwa kufanya hivyo lakini anastaajabu
Amedai kuwa watu aliowaorodhesha waingie mahakamani wamezuiliwa kuingia; “Nakala ninayo sasa majaji leo wakati nimeletwa Mahakamani katika watu nimewaandika waruhusiwe mmoja amekatazwa asiingie.”
Akiisoma orodha hiyo amemtaja Dk. Stephen Linco aliyesafiri kutoka Ujerumani kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo aliyekuwa namba 12 kwenye orodha hiyo, “Mwingine Cathe kutoka Washngton Marekani nae amezuiliwa hapo nje.”
Lissu ameiambia mahakama hiyo kuwa wapo wanachama na wananchi waliotaka kuingia kusikiliza shauri hilo wamezuiliwa kwenye malango ya kuingia mahakamani hapo.
“Mimi nataka kujua hii ni mahakama ya mapolisi au mahakama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anayeamua mtu aingie au asiingie ni nani, mapolisi au mahakama?” amehoji Lissu.
Jambo la Pili Lissu alieleza mahakama hiyo kuwa alitakiwa kuingia kwenye kikao cha kabla ya usikilizwaji wa shauri hilo “Jambo la pili tarehe 01 Oktoba 2025, nimeandikiwa barua tena na Msajili tena Lyakinana huyo huyo,barua hiyo imenifikia ijumaa tarehe 03/10 mchana. Subject inahusu pre session meeting. Inataka tufanye kikao Tarehe. 03 Oktoba saa nane kamili, kifupi siku hiyo hiyo ndio tukae kikao. Niliwaambia hii sio proper notice ya kikao hata kama niko gerezani masaa mawili hayatoshi kama proper notice, sikuhudhuria hicho kikao,”alidai Lissu.
Lissu aliiomba mahakama maana ya kikao hicho kisheria na kueleza kuwa barua ya mwisho ilikuwa imeambatanishwa na wito wa kuwa kesi hiyo itasikilizwa kuanzia leo tarehe 6 Oktoba mpaka 24 Oktoba halafu itaendelea Tarehe 3 hadi 11 Novemba.
“Sasa Majaji kwenye hiki cha Pre trial meeting vinatofautiana inasema itaisha Tar. 12 October. Hii kesi haijasikiliza upande hata mmoja, hamjasikiliza mashahidi hata mmoja hii Tarehe. 12 November 2025 ni tarehe ya Hukumu, kama kuna hukumu tayari tujue nani anayeandika vitu vya namma hii anapanga ratiba ya hadi hukumu itatolewa lini.” Alihoji Lissu.
Lissu aliomba ufafanunuzi wa barua hizo tatu kwa majaji wa mahakama hiyo ambapo Jaji Dunstan Nduguru baada ya kuuliza upande wa jamhuri kama wanalolote la kuzungumza kwenye hoja hizo nao wakijibu hawana akasema anaahirisha shauri hilo kwa dakika 30 kwa na wakirejea watatoa ufafanuzi.
Endelea kusoma MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Digital
ZINAZOFANANA
Msaidizi wa Mafwele aanza kutoa ushahidi kesi ya Lissu, kesho zamu yake kumbanwa
Hukumu kesi ya Mpina, INEC kutolewa Alhamisi
Mahakama yafafanua mashtaka ya Lissu kuhusu hukumu yake