October 2, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Watatu wakamatwa vurugu mwendo kasi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro

 

JESHI la polisini jijini Dar es Salaam, limewakata watu watatu kufuatia vurugu zilizozuka baada ya watu wasiojulikana kushambulia mabasi yaendayo haraka maarufu kama mwendokasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari, inaeleza kuwa watu hao wanaendelea kuhojiwa huku chanzo cha matukio hayo kikifuatiliwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo wanatafutwa.

Picha za video zilizosambaa mitandaoni hapo awali zilionyesha baadhi ya vioo vya mabasi na vituo vikiwa vimevunjwa baada ya kushambuliwa kwa mawe usiku wa kuamkia leo Jijini Dar es Salaam.

Hivi karibuni njia hiyo ya usafiri inayotegemewa na maelfu ya wakaazi wa jiji hilo kubwa zaidi nchini Tanzania imekumbwa na malalamiko ya wananchi kutokana na uhaba wa mabasi ikilinganishwa na idadi ya abiria.

Hata hivyo jumatano asubuhi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila alifanya ziara ya kushtukiza katika kituo kikuu cha mabasi ya mwendo kasi na kuwaomba radhi watumiaji wa usafiri huo na kuwataka kuwa na subira wakati serikali ikiendelea na mipango ya kutatua adha wanazozipitia ikiwemo kuongeza idadi ya mabasi.

Jumatano usiku, usiku tarehe 1 Oktoba 2025, kundi la watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe mabasi ya mwendokasi katika eneo la Magomeni na Gerezani.

About The Author

error: Content is protected !!