
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, Thabit Idarous Faina
TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza kuwa jumla ya wapiga kura 717,557 ndiyo walioidhinishwa kushiriki katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 29 2025, baada ya kukamilika kwa mchakato wa uhakiki wa daftari la kudumu la wapigakura. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Akizungumza katika mkutano na wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Jumanne, tarehe 30 Septemba 2025, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC, Thabit Idarous Faina, amesema jumla ya wapiga kura 8,325 wameondolewa katika daftari kutokana na kukosa sifa.
Kwa mujibu wa Faina, kati ya wapigakura walioidhinishwa, wanawake ni 378,334, sawa na asilimia 53, huku wanaume wakiwa 339,223, sawa na asilimia 47. Kati ya idadi hiyo, vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 35 ni 326,304 (asilimia 45), wenye umri wa miaka 36 hadi 59 ni 300,986 (asilimia 42), na walio na umri wa miaka 59 na kuendelea ni 90,267 (asilimia 13).
Pia, amebainisha kuwa ZEC imeidhinisha maeneo 50 ya kupiga kura ya mapema, ambapo Unguja kutakuwa na vituo 32 na Pemba vituo 18.
Hata hivyo, Faina amesema tayari ZEC imepokea maombi ya waangalizi wa kimataifa kutoka nchi 10 na taasisi tatu za kimataifa, huku mchakato wa mapokezi ukiendelea kabla ya kutangazwa rasmi idadi kamili ya waangalizi watakaoshiriki.
ZINAZOFANANA
Busara za Maalim Seif nguzo ya kuinusuru Zanzibar – Othman Masoud.
OMO aanza ziara ya siku saba Pemba
Polepole kumwaga mboga Jumanne