
MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dodoma, leo tarehe 25 Septemba 2025, inatarajiwa kufanyia maamuzi rufaa ya Clinton Damas (Nyundo) na wenzake watatu, waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Anaripoti Zakia Nanga, Dodoma … (endelea).
Nyundo na wenzake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani na Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Dodoma, baada ya kuwatia hatia kwenye mashitaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile, mwanamme mmoja, mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam.
Mwanamke huyo aliyetambulishwa mahakamani kwa jina la XY, ambayo maarufu “waliotumwa na Afande,” ilisikilizwa faragha ambapo upande wa Jamhuri uliwasilisha mashahidi 18 na vielelezo 12 kuthibitisha mashtaka dhidi ya watuhumiwa.
Warufaani kwenye kesi hiyo ni aliyekuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) MT. 140105 Clinton Damas, maarufu Nyundo, aliyekuwa askari magereza C. 1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson (Machuche) na Amin Lema (Kindamba).
Wakata warufani hao wanawakilishwa na mawakili watatu wa kujitegemea – Godfrey Wasonga, Roberth Owino na Meshack Ngamando – huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali, Lucy Uisso na wenzake wawili.
Washitakiwa walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, 19 Agosti 2024 na kusomewa mashtaka mawili ya kubaka kwa kundi na kumwingilia kinyume cha maumbile binti huyo.
Ilipewa Na. 23476 ya mwaka 2024 na ilisikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule.
ZINAZOFANANA
Tanesco, wadau wakutana kujadili mikakati ya kulinda vyanzo vya maji Bwawa na Nyerere
Baba Mzazi wa Askofu Bagonza kuzikwa leo
Uchaguzi mkuu ujao: Kupata au kupatwa?