
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema kuwa Chama cha ACT-Wazalendo, hakina mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wala mgombea wake mwenza, katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).
Kauli ya tume imekuja baada ya kuwapo taarifa kuwa chama hicho, kimepanga kufanya uzinduzi wa Ilani ya uchaguzi, makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam na baadaye mkutano mkuu wa uzinduzi wa kampeni za ubunge katika jimbo la Segerea, wilayani Ilala, mkoani Dar es Salaam
Tume imesema, “hakuna ratiba yoyote ya kampeni ya mgombea wa urais wa chama hicho katika eneo hilo,” na kwamba mgombea wake wa urais, Luhaga Mpina na mgombea mwenza, Fatuma Fereji, wameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho.
Mpina ameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho, i kufuatia tume kukubali pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari, tarehe 15 Septemba 2025.
Tume imekitaka ACT- Wazalendo, kuzingatia masharti ya kanuni za uchaguzi, hususan kuhusu utaratibu na ratiba za kampeni.
Taarifa ya tume imesainiwa na katibu wake, Ramadhani Kailima.
Amesema, mbali na tume kutomtambua Mpina, pia mkutano wa chama hicho katika jimbo la Segerea, haupo kwenye ratiba.
ZINAZOFANANA
Rostam ni mfano bora wawekezaji ndani na nje ya nchi-TCCIA
ACT tutavunja Tume ya Uchaguzi, tutaunda upya Jeshi la Polisi
Kesi ya Lissu kuanza kutolewa ushahidi Oktoba 6, Samia atajwa