September 23, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Othman amuaga mwanachama mwadilifu ACT Wazalendo

 

MGOMBEA Urais wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman, ameungana na viongozi wa Chama, viongozi wa dini pamoja na wananchi katika hafla ya kuuaga mwili wa Hawa Moses Kulola maarufu kama Pembe la Ng’ombe, iliyofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja, Mjini Magharibi Unguja. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Marehemu Pembe la Ng’ombe, ambaye alikuwa mwanachama na muhamasishaji mashuhuri wa ACT Wazalendo, alifariki dunia jana tarehe 21 Septemba 2025 katika Hospitali ya Kivunge, Kaskazini Unguja, mara baada ya kuanguka ghafla katika mkutano wa hadhara kijijini.

Akizungumza katika tukio hilo, Mgombea Urais Othman Masoud alieleza kuguswa kwake na msiba huo mkubwa, akiwasihi ndugu wa marehemu kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu.

Alisema marehemu alikuwa mstari wa mbele muda wote katika kupigania haki na demokrasia, akibeba sauti ya wananchi na kupinga dhulma.

Othman alisisitiza kuwa njia pekee ya kumuenzi Pembe la Ng’ombe ni kuendeleza mapambano ya kudai mabadiliko na demokrasia ya kweli Zanzibar.

Alitoa wito kwa wanachama wa ACT Wazalendo na wananchi kwa jumla kuungana katika harakati za kuleta Zanzibar mpya yenye usawa na heshima kwa kila mmoja.

About The Author

error: Content is protected !!