
Tundu Lissu akiwa mahakamani
MAHAKAMA Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imepanga kutoa uamuzi mdogo kwenye kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu Jumatatu ya tarehe 22 Septemba 2025, majira ya saa tatu asubuhi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(vendelea)
Uamuzi huo unakuja kufuatia Lissu kuweka mapingamizi kuhusiana na ubovu wa hati ya mashitaka pamoja na maelezo ya mashahidi (witness statement) kuchukuliwa kinyume cha sheria na pia yapo maelezo ya mashahidi ambao mahakama ilisema utambulisho wao ufichwe wameshindwa kufanya hivyo.
Lissu aliwakilisha mapingamizi hayo baada ya kusomewa mashtaka, kufuatia kutupiliwa mbali pingamizi lake la awali juu ya mapungufu ya kisheria yaliokuwa kwenye Committal process, iliyosomwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Baada ya siku kadhaa za mabishano ya hoja za kisheria na rejea za kesi mbalimbali kati ya mshtakiwa na Mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga hatimaye leo, Alhamisi tarehe 18 Septemba 2025, Mahakama imehitimisha kusikiliza mapingamizi hayo.
Endapo Mahakama chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru wanaosikiliza kesi hiyo wakikubaliana na hoja za mshtakiwa inawezekana kesi hiyo ikafutwa, kama mapingamizi hayo yatatupiliwa mbali kesi ya msingi itaendelea kwa mshtakiwa kusomewa makosa yake kisha akatae au kukubali.
ZINAZOFANANA
Polepole awapa somo jipya polisi
Lissu agoma kuendelea na kesi hadi wafuasi wake waingie mahakamani
Jeshi la Polisi liwaachie wale wote waliokamatwa Mahakamani leo