HATIMAYE Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imepitisha na kuwapa ridhaa ya kuwania urais wagombea 11 wakaopambana katika kinyang’anyiro kitakachofanyika tarehe 29 Septemba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).
Taarifa iliyotolewa jana, tarehe 11 Septemba 2025 na Mwenyekiti wa ZEC Jaji George Joseph Kazi walioteuliwa ni Hussein Juma Salim (TLP), Ameir Hassan Ameir (Chama cha Makini), Hamad Mohammed Ibrahim (UPDP), Leila Rajab (NCCR-Mageuzi), Mfaume Khamis Hassan (NLD) na Mgau Kombo Mgau (NRA).
Wengine ni Dk. Hussein Ali Mwinyi (CCM), Othman Masoud Othman (ACT-Wazalendo) Hamad Rashid Mohammed (ADC) Juma Ali Khatib (ADA TADEA) na Said Soud (AAFP).

Tangazo hilo la ZEC, linahitimisha majadala uliokuwa ukizagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Othman Masoud Othamn (OMO) ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, ameenguliwa kuwania nafasi hiyo kwa sababu ya kutokidhi vigezo zinavyotakiwa.
Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa mchuano mkali utakuwa kati ya Dk. Mwinyi na OMO kutokana na wato kuwa na ushawishi mkubwa kwenye jamii na wote wako kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 2010, mgombea urais anayeshika nafasi ya pili huwa Makamu wa Kwanza wa Rais.
ZINAZOFANANA
Mpina ashinda kesi, mahakama yamruhusu kurudisha fomu
Takukuru yaonya wagombea wanaolipuka na ahadi za kampeni
Mahakama kuamua hatma ya Lissu Jumatatu