
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, itatoa uamuzi wa maombi madogo yaliyowasilishwa kwenye shauri la mgawanyo wa raslimali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuomba nyaraka za vikao mbalimbali pamoja na taarifa za fedha ya chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kwenye shauri hilo walalamikaji ni Said Issa Mohamed, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema- Z’bar, Maulida Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis wajumbe wa bodi ya wadhamini ya chama hicho.
Leo tarehe 10 Septemba 2025, mbele ya Jaji Hamidu Mwanga, walalamikaji waliibua maombi mapya yalipewa Na. 20585/2025 ya kuomba nyaraka mbambali za chama hicho.
Nyaraka hizo ni pamoja na muhtasari wa vikao vya bodi ya wadhamini, vikao vya Sekretarieti ya kamati maalum Zanzibar, nyaraka la tamko la mali na nyaraka za fedha za benki (Bank Statement) na taarifa ya ukaguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya Chadema.
Upande wa wajibu maombi ‘Chadema’ uliowakilishwa na Wakili Hekima Mwasipu uliyapinga maombi hayo na kueleza hoja za kwa kuzishikamanisha na sheria.
Nje ya Mahakama Katibu Mkuu wa chama hichi, John Mnyika, amedai kuwa chama hicho kitapinga maombi hayo.
“Hawa walalamikaji wanamadai matatu dai la kwanza wanachokiita mgawanyo usiosawa wa raslimali, dai la pili wanadai kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia kwenye chama dai la tatu wanadai chadema wanatoa maoni ya kuvuruga msimamo kwa hiyo nilikuwa nataka kutoa ufafanuzi juu ya madai yao.”
“Leo wameomba maombi nyaraka za tangu 2019 mpaka 2024 kwa kipindi chote kwa hiyo ni wigo mpana wa nyaraka.”
Mnyika amesema kuwa hoja za Chadema zilijikita kwenye mantiki yamaombi yao na kuwa mahususi “hawajasema kikao kipyi mahususi kwa kikao kipi wameomba nyaraka bila kufuata misingi ya sheria.”
Mnyika amesema kuwa waombaji hao wameomba nyaraka ambazo hazipo kwenye Mamlaka ya Chadema “kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa chama cha siasa kinatakiwa kipeleke nyaraka kwa msajili wa vyama vya siasa msajili ndio mwenye hizo nyaraka wangetumia utaratibu wa kumuomba Msajili, lakini hata nyaraka za CAG ni nyaraka za umma kwa maoni yangu wamefanya hivyo ili kuchelewesha haki”
Mnyika amedai kuwa waombaji wameomba orodha ndefu ya nyaraka kwa bahatisha jambo ambalo halifanyiki kwenye sheria.
Mahakama hiyo itatoa uamuzi kuhusu maombi hayo tarehe 29 Septemba 2025.
ZINAZOFANANA
Rais Samia azidi kumwaga ahadi Igunga
Lissu: Mahakama hii haina uhalali, Mahakama ya Kisutu imevuruga mchakato
Kingu amshukia Humphrey Polepole